KATIKA hali isiyo ya
kawaida watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameficha bunduki kwenye kichaka
kilichopo eneo la shule ya Msingi mbuyuni iliyopo kata ya mbuyuni manispaa ya
Morogoro.
Bukundi hiyo yenye namba MG 6360 A iliokotwa eneo la
shule hiyo iliyopo mtaa wa MagulumbasiShuhuda wa tukio hilo ambaye ndiye aliyeiona bunduki
hiyo Bw Kasimu Athuman alidai kwamba wakati akikata miti kwenye kichaka hicho
aliiona bunduki hiyo ikiwa imefichwa na majani
Bw Kassim Athumani ambaye
ndiye aliyeiona bukundi hiyo.Akielezea zaidi alisema niliamua kuja kukata miti kwenye kichaka na ndipo
nilishuhudia bunduki ikiwa imeficha eneo la kichaka hiki,na kwamba baada ya
kuiona niliacha kazi hiyo na kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa
huu
Mwenyekiti wa Mtaa wa
Magulumbasi kata ya Mbuyuni manispaa ya Morogoro.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huyo Bw Salum
Kimanga alipohojiwa na mwandishi wa habari hizi alidai kwamba baada ya kupokea
taaria za uwepo wa bunduni hiyokwenye mtaa wake naye alitoa taarifa kwa diwani
wake
,”Baada ya mkazi wa mtaawangu Bw Athumani kunipa
taarifa hizo nilifika eneo la tukio na kushuhudia bunduki hiyo name nilitoa
taarifa kwa bosi wangu diwani wa kata yetu” alisema mwenyekiti
huyo.
Alipotakiwa kueleza mazingia ya tukio hilo
mwenyekiti huyo alidai kwamba huenda majambazi ndio walioficha bukudni hiyo
kwenye eneo hilo la shule.
Sehemu ambayo Bw Athuman
alikuwa akikata miti na baade kustuka baada ya kuiona bunduki hiyo kwenye
kichaka hicho
Polisi walifika eneo la tukio
na kuelekea kwenye kichaka hicho wakiongzwa na mwenyekiti wa Mtaa
huo
Polisi wakishangaa baada ya kuiona bunduki hiyo
Polisi hao wakiichukua bunduki hiyo
Polisi
wakiikagua bunduki hiyo inayosadikiwa kufichwa eneo hilo na
majambazi
Diwani wa kata ya Mbuyuni
Samwel Msuya[wakwanza kulia] ambaye alifanya jitihada kumbwa kutoa taarifa kwa
mwandishi wa mtandao huu pamoja na jeshi la polisi
mfuko wa bunduki hiyo uliandikwa namba hizo 5148
Bunduki yenye iliandikwa namba hizo MG 6360 A
Polisi
wakiondoka eneo la tukio na bunduki hiyo jana jioni.
Afisa mmoja wa polisi aliyekuwepo eneo hilo ambaye
aliopa hifadhi ya jina lake alipotakiwa kueleza tukio hilo alidai kwamba
wanafanya uchunguzi wa tukio hilo kwa lengo la kubaini kama bunduki hiyo
ilishahusika kwenye matukio ya ujambazi ndani ya nje ya mkoa wa
morogoro. NA DUSTAN
SHEKIDELE,
Post a Comment