Dhumuni la mkutano huu, ni kutoa ufafanuzi/maelezo ya Mpango mpya wa kujiunga na JKT (Compulsory programme) kwa wanafunzi watakaohitimu Kidato cha Sita 2013. Mpango ambao uliwahi kuwepo hapo awali. Pia utawahakikishia fursa ya kufafanuliwa maswali na dukuduku zenu.
Ikumbukwe kwamba Vijana wamekuwa wakishirikiswa katika suala la ulinzi wa Jamii zao tangu enzi za kabla ya Uhuru. Kwa mfano Wayao(Ndagala), Wamakua(Mmera), Wagogo(Ikumbi), Wanyaturu(Misanga), Wamasai(Manyata) n.kMafunzo hayo katika makabila mbalimbali yalikuwa yakitolewa wakati wa mafunzo ya Jando na UnyagoMafunzo yaliyotolewa katika makambi hayo yalihusu ukakamavu, uhodari katika kufanya kazi za kilimo na ufugaji, ulinzi , nidhamu, ushujaa na adabu njema na malezi ya familia.Nchi mbalimbali pia zimekuwa na program za kuwaandaa vijana wake. Kwa mfano Zambia ( National Service), Kenya ( National Youth Service), Ghana ( National Service Scheme), China (Poverty Alleviation Relay Project), New Zealand ( Conservation Corps), Nigeria ( National Youth Service), Namibia ( National Youth service), Malaysia ( National Youth Scheme), Israel (National Youth Scheme) n.kNchi mbalimbali ikiwemo Msumbiji, Afrika Kusini, Rwanda zimeshatuma wawakilishi wao kutembelea JKT kujifunza jinsi ya kuanzisha mafunzo kama hayo katika nchi zao.Aidha, Sera ya Ulinzi na Usalama wa nchi yetu inatamka bayana kwamba wajibu wa kuilinda nchi yetu ni ya Mwananchi wenyewe na hasa ninyi Vijana.

Ninyi vijana hamtokuwa wa kwanza kupitia katika program hii, kwani Watanzania wengi wakiwemo Viongozi wa Idara za Serikali, Mashirika ya Umma, Wakurugenzi, Viongozi katika Asasi binafsi na hata Viongozi wa Kitaifa ( Mawaziri Wakuu na Ma-Rais) pia walifaidika na mpango huo
Wazo la kuanzisha
JKT katika Tanzania lilijadiliwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa mwaka wa Umoja wa Vijana wa TANU ( T.Y.L) uliofanyika mjini Tabora, mwaka 1962.19 Apr 63 Baraza la Mawaziri liliidhinisha kuanzishwa kwa mpango huo baada ya kufanya marekebisho yaliyohitajika.Mnamo tarehe 10 Jul 63 JKT ilianzishwa rasmi kwa kuandikishwa vijana 11 kutoka Wilaya 11. Vijana hao wa mwanzo walikuwa Makatibu wa Umoja wa Vijana katika Wilaya zao.Kukua kwa JKT (1963 – 1994)Vijana wa kujitolea waliendelea kuongezeka kwa ajili ya kupata mafunzo ya uzalendo, ujasiriamali na Uongozi.



Ni matarajio ya Serikali kwamba, mtapokea wito huu kwa dhati na ari kubwa na kwamba mtashiriki kwa uaminifu na uhodari mkubwa.Aidha, kwa upande wetu JKT, tunategemea Ushirikiano wenu katika kuitikia wito huu wa Serikali kwa kuripoti kwa wakati makambini.Pia kwa upande wetu wa JKT, tunaahidi kuwapokea na kutekeleza mafunzo ya JKT kwa weledi mkubwa.Tunaahidi kwa niaba ya Uongozi mzima wa JKT na Wizara kwa ujumla, kwamba mafunzo yataratibiwa kitaalamu bila kuathiri maisha ya wanafunzi.Maandalizi yote ya msingi kwa ajili ya mafunzo yenu yameshakamilika na kinachosubiriwa kwa sasa ni ninyi kuripoti makambini.Haki zenu za msingi kama vile posho, malazi,chakula, matibabu, maji, na burudani n.k.) zitaratibiwa ipasavyo.Lakini pia, tungependa tuwakumbushe kwamba, sheria ya wito wa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria bado ipo na haijafanyiwa marekebisho, kwa hiyo ni wajibu wa kila anayepaswa kujiunga na mafunzo hayo, kutekeleza jukumu hilo bila kusita.HITIMISHOAsanteni sana kwa Kunisikiliza
Source: http://jkt.go.tz/mada-ya-vijana-wa-mujibu-wa-sheria.h
Post a Comment