Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Hospitali ya taifa ya Muhimbili yaadhimisha miaka 13 huku ikikabiliwa na changamoto tele.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali wa Serikali, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donald Mmbando akitoa hotuba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dk. Hussein Mwinyi wakati wa kufungua rasmi maonyesho ya huduma za hospitali ya taifa ya Muhimbili katika kuadhimisha miaka 13 ambapo amezungumzia nia ya serikali kusaidiana na hospitali hiyo katika kutafutia ufumbuzi changamoto zinazoikabili ili iweze kuendelea kutoa huduma kwa wananchi katika kiwango cha juu kama ilivyokusudiwa.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali wa Serikali, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donald Mmbando (katikati waliokaa)katika picha ya pamoja na wakuu wa idara mbalimbali na wajumbe wa bodi ya wadhamani mara baada ya kufungua rasmi maonyesho ya huduma za hospitali ya taifa ya Muhimbili katika kuadhimisha miaka 13 na miaka mitatu kama hospitali ya ubingwa wa Juu ya taifa.

*******
Serikali ya Tanzania imepongezwa kwa juhudi zake ilizofanya na inazoendelea kufanya kwa sasa katika kuhakikisha kwamba majukumu makubwa matatu ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili yanatekelezwa ipasavyo.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya huduma za hospitali ya taifa ya Muhimbili katika kuadhimisha miaka 13 kama hospitali ya taifa na miaka mitatu kama hospitali ya ubingwa wa juu ya taifa uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya hospitali hiyo imesema kwa upande wa tiba imefanikiwa kuongeza idadi ya vitanda kuwa 1271, na kuongeza idara na kuwa 30.
Hospitali hiyo imesema majukumu yake makubwa matatu ni pamoja na kutoa matibabu ya rufaa ya juu  (superspecialist services) kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kiwango cha juu cha ubora.
Majukumu mengine yametajwa kuwa ni kufundisha wanafunzi wa kada mbalimbali za afya kutoka vyuo vikuu vya udaktari vilivyopo nchini kwa sasa na kufanya utafiti katika Nyanja za sayansi ya tiba na afya, tafiti ambazo zitaboresha huduma ya tiba kwa wagonjwa.
Hata hivyo imesema inakabiliwa na changamoto kadhaa kama vile Uwezo wa kifedha, Sera ya Msamaha, tatizo la madawa, upungufu wa wafanyakazi hasa katika kada ya wauguzi na pia wataalamu katika maeneo muhimu ya kibingwa, uchakavu wa vifaa na msongamano wa wagonjwa.

(Na.Mo Blog Team)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top