Ofisa wa
Matibabu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Yasinta Shibola akitoa
ufafanuzi kwa watu mbambali waliotembelea banda la NSSF wakati wa maonesho ya
Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam leo ambapo NSSF ni
moja ya taasisi zinazoshiriki katika maonesho hayo.
Baadhi ya
watu mbalimbali wakipata maelezo ya huduma zinazotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF) na hasa huduma ya mafao ya matibabu iliwafutia watu wengi,
wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es
Salaam.
Ofisa
Uhusiano Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Maife
Kapinga akifafanua jambo kuhusu huduma ya mafao ya matibabu wakati wa maonesho
ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam
jana.
Baadhi ya
watu waliojitokeza katika banda la NSSF wakipata maelezo ya huduma mbalimbali za
NSSF.
Na
Mwandishi Wetu
WATANZANIA
wametakiwa kujiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili
kufaidika na huduma za bure katika mafao yanayotolewa na shirika
hilo.
Wito huo
umetolewa leo na Ofisa wa matibabu wa NSSF, Yasinta Shibola, jijini Dar es
salaam katika maonesho ya siku tatu ya Muhimbili kutimiza miaka 13 toka
kupandishwa hadhi ya kuwa hospitali ya Taifa tangu mwaka
2000.
Shibola
alisema kuwa NSSF hawatoi mafao ya kustaafu pekee bali wana mafao mengine ambayo
hutolewa bure kwa mwanachama aliyejiunga na mfuko
huo.
“Mafao yetu
yamejikita kusaidia wateja wa sekta binafsi na wa serikali, lakini pia hata wale
wanaofanya kazi kwa kujitegemea kama atakuwa mwanachama wetu atapatiwa fao hilo
kama wengine tena katika hospitali atakayochagua yeye mwenyewe katika zile
ambazo tumeingia nazo mkataba na kupewa fao hilo kama wengine wote, hakuna
upendeleo hapo,”alisema
Naye Ofisa
habari wa NSSF, Maife Kapinga, alisema kuwa fao la matibabu (SHIB) ni bure na
linahudumia watu wanne katika familia moja.
Kapinga
alitoa wito kwa watanzania kujiunga na shirika hilo ili wafaidike na mafao
yanatolewa bure



Post a Comment