Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Jana ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka 23 ya ajali ya ndege ya Chipolopolo


 
imageimageimageimageimageIlikuwa tarehe kama ya leo miaka 23 iliyopita wakati ndege iliyokuwa imebeba wachezaji 18 wa kikosi cha timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo , watu wa nne wa benchi la ufundi akiwepo kocha mkuu wa timu hiyo Godfrey Ucar Chitalu na wasaidizi wake watatu , na viongozi watatu wa chama cha soka cha Zambia ilipopata ajali mbaya kwenyenpwani ya Gabon na kuua watu wote 30 waliokuwemo .

Ndege hiyo aina ya DHC-5D Buffalo ikiwa na namba za usajili (AF-319) ilianguka na kuzama kwenye bahari ya Atlantic karibu kabisa na pwani ya mji mkuu wa Gabon Libreville baada ya matatizo ya kiufundi . Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na jeshi la Gabon ndege hiyo ilipata hitilafu iliyosababisha moto kwenye moja ya Injini zake hali iliyomlazimu rubani Kanali Fenton Mhone kuizima injini hiyo , hata hivyo Rubani alikosea na kuzima injini nyingine iliyokuwa nzima hali iliyofanya ndege hiyo kushindwa kwenda vizuri na hatimaye kuanguka baharini .
Zambia ilikuwa njiani kuelekea Senegal ilikokuwa inaenda kucheza na timu ya taifa hilo katika michezo ya hatua za mwisho ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 1994 huko Marekani .
Moja ya watu waliosalimika kwenye ajali hiyo alikuwa nyota wa enzi hizo wa timu ya taifaya Zambia Kalusha Bwalya ambaye hii leo ni Rais wa chama cha soka cha Zambia FAZ ambaye alichelewa safari hiyo abapo alikuwa anatokea nchini Uholamzi alikokuwa anacheza soka la kulipwa .
Ajali hii ndio ajali mbaya kuliko zote kwneye historia ya soka la Zambia na iliilazimu nchi hiyo kuunda timu mpya kwa haraka ambayo iliongozwa na Kalusha Bwalya.
Cha kushangaza ni kwamba timu mpya iliyoundwa kwa haraka haraka iliweza kufuzu kucheza kombe la mataifaya Afrika mwaka uliofuatia ambapo ilifika fainali ilikofungwa na Nigeria 2-1.
Hadi leo kikosi hicho ambacho kilikuwa na wachezaji maarufu kama Kipa Efford Chabala , beki Eston Mulenga ,kiungo Moses Chikwalakwala na mshambuliaji Patrick ‘The Bomber Banda kinaaminika kuwa kikosi bora kilichowahi kutokea kwenye soka la Zambia na wengi walitarajia kukiona kiiwakilisha Afrika kwenye fainali za kombe la dunia Maka 1994.
Kocha wa timu hiyo Godfrey Ucar Chitalu alipata umaarufu mkubwa enzi zake akiwa mshambuliaji wa klabu ya Kabwe Warriors ambapo aliwahi kuweka rekodi a kufunga mabao 117 kwenye msimu wa mwaka 1972 rekodi ambayo FIFA imegoma kuitambua . Rekodi hiyo ilitajwa san
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top