Meneja mahusiano ya
nje-Vodacom Tanzania,Salum Mwalimu akifafanua zaidi kuhusiana na udhamini wa
kampuni hiyo kwenye tamasha la soka la kuadhimisha sikukuu ya Wafanyakazi
nchini,ambapo timu kumi 14 zimepangwa kushiriki.Kulia ni Ofisa Udhamini na
Matukio Bwa.Kaude Ibrahim,Mkuu wa Idara ya Michezo-Clouds Media Group
Shaffih Dauda na mwisho kabisa kushoto ni Mwakilishi kutoka THT ambao pia
watashiriki kutoa burudani kwa ujumla.
========= ======== ======
Timu 14 kushiriki tamasha la Mei Mosi
Tamasha la soka la
kuahimisha sikukuu ya wafanyakazi nchini litafanyika siku ya jumatano (Mei Mosi)
kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini.
Tamasha hilo lililoandaliwa
na kampuni ya Butterfly Advertizing and Marketing kwa kushirikiana na Sports
Extra and Sports Bar , litashirikisha jumla ya timu 14 za makampuni mbalimbali
ya hapa jijini kwa mujibu wa mratibu wake, Shafii Dauda.
Dauda alizitaja kampuni
hizo kuwa ni Benki ya CRDB, NMB, Vodacom Tanzania, Clouds Media group, Infinity
Communications, Tanzania Cigarette Company (TCC), NSSF, TBL, Tanesco, National
Housing Corporation (NHC), Simbanet, Fastjet, Umoja Water
na DHL.
Alisema kuwa Vodacom
Tanzania na NMB ndiyo wadhamini wakuu wa tamasha hilo lililopangwa kuanza saa
3.00 asubuhi na kupambwa na bendi ya Sky Light na Tanzania House of Talent
(THT).
Kwa mujibu wa Dauda, timu
hizo zitagawanywa katika makundi manne na kucheza kwa mchezo wa ligi na mshindi
wa kwanza na wa pili wa bonanza hilo watazawadiwa vikombe na timu nyingine
shiriki zitapewa vyeti.
Alisema kuwa sababu kubwa
ya kuandaa bonanza hilo lililopangwa kumalizika saa 2.00 usiku ni kuwakusanya
pamoja na kubadilishana mawazo wafanyakazi katika siku yao hiyo
muhimu.
Meneja Uhusiano wa Nje wa
Kampuni ya Vodacom, Salum Mwalimu alisema kuwa sababu kubwa ya kudhamini na
kushiriki katika bonanza hilo ni kuwapa zawadi wateja wao kwani
wanaaminikuwa timu zote shiriki ni wateja
wao.
“Mbali ya kudhamini, sisi
tutashiriki na timu yetu, tunataka kuwaonyesha kuwa hata soka nasi tunacheza,
tunawataka mashabiki kufika kwa wingi kwani ni hakuna kiingilio,” alisema
Mwalimu.
Post a Comment