Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LIGI KUU BARA: YANGA V MGAMBO MKWAKWANI, MTIBWA VS OLJORO MANUNGU, KAGERA VS TOTO KAITABA, MOTO UTAWAKA LEO!


mgambo vs yanga
 
Ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2012/2013 inatarajiwa kushika kasi leo hii katika miji ya Tanga, Kagera na Morogoro.
Vinara wa ligi hiyo, Dar Young Africans wana kibarua kizito mbele ya maafande wa Mgambo JKT katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.
Kuelekea katika mchezo huo timu zote zimejigamba kuibuka na ushindi ili kupata mzigo wa pointi tatu muhimu.
Afisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema maandalizi yote yamekamilika na wachezaji wote wapo salama.
“Tunahitaji ushindi ili kujihakikishia zaidi nafasi ya kunyakua taji msimu huu, tunajua Mgambo wanahitaji pointi tatu kutoka kwetu ili kujinisuru na mkasi wa kushuka daraja lakini tuko sawa kupambana nao”. Alisema Kizuguto.
Nao Mgambo kupitia kwa katibu mkuu wake Antony Mgaya alisema wamejiandaa kwa leongo moja tu la kupata pointi tatu na kuendeleza umwamba kwa klabu kubwa kwa sasa nchini Tanzania.
“Heshima ni kitu cha maana kwa klabu, lakini pointi tatu ni lazima kwetu na ndio maana tuko kamili kuwakabili Yanga katika uwanja wetu ambapo imani yetu ni mashabiki wengi kufika kutushangilia”. Alisema Mgaya.

Mbali na kipute hicho cha Tanga, Mkaoni Kagera katika dimba la Kaitaba, wana “Nkulukumbi” Kagera Sugar watakuwa na kibarua kizito jioni ya leo dhidi ya vijana wa mitaa ya Kishamapanda Toto African.
Kocha mkuu wa Kagera Abdallah Kibadeni “King Mputa” alisema wanajiandaa kwa mara nyingine kuwaoneshea ubabe wapinzani wao kwani mechi ya mzunguko wa kwanza waliwafunga mabao 2-1 katika dimba la CCM Kirumba.
“Tumejiandaa kupata pointi tatu ili kujiimarisha katika nafasi ya tatu ambayo tunapambana na Simba, Toto tunawajua sana na lazima wafungwe”. Alisema Kibadeni.
Kwa upande wa Kocha wa Toto na meneja wa uwanja wa CCM kirumba, John Tegete alisema hana cha kupoteza mbele ya Kagera, kikubwa ni kupigania pointi tatu ili kusonga mbele na mapambano ya kujinusuru na mkasi wa kushuka daraja.
“Tuliwabana Mtibwa kwao na kupata pointi tatu, sasa tumerejea kanda ya ziwa kupambana na ndugu zetu kwao Kaitaba, wana kocha mzuri na wachezaji wazuri, lakini sisi pia hatujambo, tuko barabara kupigania uhai wa kusalia ligi kuu”. Alisema Tegete.
Huko Mkoani Morogoro katika dimba la Manungu, Mtibwa sugar watakuwa na kibarua kizito mbele ya maafande wa JKT Oljoro.
Tobias Kifaru Lugalambwike, msemaji wa klabu ya Mtibwa alisema baada ya kupata sare ya 2-2 na Toto mechi iliyopita, sasa wanajipanga kupata matokeo mazuri dhidi ya maafande hao wa jeshi.
“Oljoro wamejeruhiwa baada ya kufungwa 3-0 na Yanga, leo hii watatoneshwa zaidi kidonda kutokanana na maandalizi mazuri tuliyofanya kwa ajili ya mchezo huu, mashabiki wetu wasiogope, tuko vizuri sana”. Alisema Kifaru.
Kwa upande wa Oljoro, kocha msaidizi wa klabu hiyo Riziki Shawa alisema hesabu zao ni kuwafunga mtibwa ingawa soka lina matokeo ya aina tatu, kifunga, kufungwa na kutoa sare, tukipata yoyote kati ya hayo watamshukuru Mungu.
“Kazi si nyepesi hata kidogo, wapinzani wetu huwa wanacheza soka zuri na wakiwa Manungu wanajua kupambana, lakini tuko sawa na wachezaji wote wapo salama”. Alisema Shawa.
 
(Na Baraka Mpenja wa fullshangwe Dar es salaam)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top