Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LOWASSA KUKABIDHIWA TUZO YA HESHIMA IRINGA JUMAPILI

MH.EDWARD LOWASSA
askAskofu Dkt Boaz Solla akiwa na waumini wake
Na  Francis Godwin   ,Iringa
WAUMINI  na uongozi  wa  huduma   ya injili na  uponyaji  ya Overcomers Power Center  (OPC) chini ya Askofu Dkt Boaz Sollo inategemea  kumtunuku  tuzo ya  heshima kwa mchango  wake mkubwa katika Taifa waziri mkuu  mstaafu  wa jamuhuri ya  Muungano  wa Tanzania Edward Lowassa katika  hafla  maalum  itakayofanyika  siku ya  jumapili mjini  Iringa .
Waumini  hao  wameandaa maandamano makubwa  ya amani  kwa  ajili ya  kumpokea Lowassa  kutoka  katika  uwanja  wa Ndege Nduli  majira ya saa 3 asubuhi  atakapowasili kwa Ndege na  kuelekea katika  ukumbi  wa St Dominic ambako kutafanyika  shughuli  hiyo kuanzia muda wa saa 6 mchana .
Akizungumza na  waandishi  wetu  askofu Dkt Sollo  alisema  kuwa mbali ya  kumtunuku tuzo  hiyo  Bw  Lowassa pia  kiongozi  huyo anataongoza  harambee  ya  kuchangia ujenzi wa  jengo la kanisa  la OPC linaloendelea  kujengwa katika  eneo la  zizi la Ng’ombe ambapo  zaidi ya  Tsh. Milioni 250 zinahitajiika kukamilisha  ujenzi  wa  jengo hilo  pamoja na kituo cha Radio   Overcomers Fm (98.6 Mhz)kilichopo mjini Iringa .
Dkt  Sollo  alisema  kuwa  lengo la  OPC  kumwalika na kumtunuku  tuzo ya  heshima  Bw  Lowassa ni  kutokana na kuwa  jirani  zaidi na jamii na amekuwa akiitika  wito  wa makundi mbali mbali  na kuyasaidia bila  ubaguzi  wowote  hivyo kutokana na mchango  wake  huo kwa jamii wao  kama kanisa wameona ni  vema  kuutambua mchango  wake huo na kumwalika  ili kumpa tuzo hiyo maalum kama ahsante kwake.
“ Tuzo  hiyo  itampa moyo  zaidi  wa kuendelea  kuwa karibu na jamii na  kutambua pia mapokeo ya  jamii ambayo amekuwa akiisaidia mara kwa mara ….ikiwa ni  pamoja na  kuendelea  kusaidia  kuendeleza amani nchini kwa kuchangia nyumba  za ibada”
Pia  alimtaka Lowassa  kuendelea  kusaidia  jamii bila  kuchoka hata kama baadhi ya  watu  wasiopenda jitihada zake  kuendelea   kutoa maneno yenye  kumkatisha tamaa na kuwa siku  zote kile anachokifanya  jamii inakitambua na Mungu ndie ajuaye na ndie mtoa baraka kwake.
Dkt  Sollo  alisema  kuwa Lowassa ambae ni mbunge  wa  jimbo la Monduli mkoani Arusha  amekuwa kipenzi cha  wengi hata  wale  wasio wapiga  kura  wake na  kuwa  uongozi  wake kama  waziri  mkuu  wengi  walitokea  kumpenda na kuwa toka alipojiuzulu nafasi  hiyo ya  uwaziri mkuu  hajapata  kufika mkoani Iringa  hivyo sehemu kubwa ya  wana Iringa  wana hamu  kubwa ya  kukutana nae kwa mara  nyingine.
Hata  hivyo  baadhi  ya  wakazi  wa Manispaa ya  Iringa  wamepongeza  hatua ya OPC chini ya Dkt Sollo kuamua  kumtunuku  tuzo  hiyo Lowassa na  kuwa ni kweli anastahili  kupewa  tuzo kwani ni  miongoni mwa viongozi  waadilifu na  wachapa kazi hapa nchini.
Anania  Sanga  alisema  kuwa  kuna kila  sababu ya  viongozi kama  Lowassa kuendelea  kuthiaminiwa kama  ambavyo OPC ilivyoamua  kuutambua  mchango  wake kwa  kukusudia  kumtunuku tuzo hiyo maalum ambayo  si heshima kwa  kituo hicho  cha OPC pekee  bali ni heshima ya  mkoa  wa Iringa ni mfano  kwa  viongozi  wengine  kufanya kazi  ya jamii  kwa ufanisi zaidi  ili  kuja  kupongezwa na jamii kama  hivyo .
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top