
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Juma Ameir Hafidh, akifungua mafunzo ya siku nne juu ya utekelezaji Utafiti wa hali ya Utumishi Nchini, kulia kwake ni Kamishna wa Idara ya Mipango ya Watenda kazi katika ofisi hiyo Seif Shaban Mwinyi. 

Kamishna wa Idara ya Mipango ya Watenda kazi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Seif Shaban Mwinyi, akitoa nasaha kwa washiriki wa mafunzo ya utekelezaji Utafiti wa hali ya Utumishi Nchini kutoka Tasisi za Serekali na zile za Binafsi, huko katika ukumbi wa ZSSF Kilimani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 

Mratibu wa Utafiti kutoka Ofisi ya Takwimu Bi. Khadija Khamis Hamad akifafanua jambo juu utafiti utakao fanywa, kulia Nassra Humuud Salum mshiriki wa mafunzo kutoka Wizara ya Kazi na kushoto Umrat Suleiman Muh’d Ofisa Mipango Fedha, Uchumi Zanzibar.

Mhariri Mkuu wa ZBC TV Yussuf Yussuf Khamis kulia akimuliza swali Kamishna wa Idara ya Mipango ya Watenda kazi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Seif Shaban Mwinyi juu ya maandalizi ya Utafiti huo huko katika ukumbi wa ZSSF Kilimani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
(PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR).


Post a Comment