Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania Prof. Benno Ndulu akijibu hoja kwa ujumbe wa Benki ya Dunia huku Waziri
wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akimsikiliza kwa
makini.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Bw.
Makhtar Diop aliyekaa katikati, akitoa ufafanuzi wa mikakati wa vipaumbele
hivyo. Kutoka kushoto ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda,
Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier na kulia ni Mkurugenzi wa Sekta ya
kupunguza umasikini na masuala ya Uchumi kanda ya Afrika Bw. Marcelo
Giugale.
Ujumbe wa Tanzania
pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia wakijadili namna ya kuendeleza na kuboresha
sekta mbalimbali zilizopewa vipaumbele kwa Tanzania ambavyo ni pamoja na
Nishati, Usafirishaji na masuala mazima ya
MKUKUTA.
Kutoka kushoto ni
Meneja wa Ubinafsishaji Sekta ya Maendeleo kanda ya Afrika Bi. Irina Astra Khan,
Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser akijibu hoja
katika majadiliano hayo. Kulia ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania,
Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akisikiliza kwa
makini.
Ujumbe wa Tanzania
ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akitoa ufafanuzi wa
vipaumbele kwa ujumbe wa Benki ya Dunia.
Kutoka kushoto ni
Mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Dickson Lema, Mchumi wa BOT Bi. Haika
Mbaga, Kaimu Balozi Ubalozi wa Tanzania Washington DC Bibi Lily Munanka,
Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor na Mchumi
wa BOT Bi. Sauda Msemo wakifuatilia majadiliano hayo.
Kutoka kushoto ni
Mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrick Pima, Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais
Tume ya Mipango Prof. Longinus Rutasitara, Afisa Mwambata
anayeratibu masuala ya uchumi, biashara na uwezeshaji ya Benki ya Dunia na
Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Paul Mwafongo wakiandika majadiliano hayo.
Kutoka kushoto ni
Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser, Meneja wa
Social Protection kanda ya Afrika Bi. Lynne D-Sherburne – Benz na baadhi ya
wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano
hayo.
Picha Juu na Chini
Wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano.Picha zote na Bi.
Ingiahedi Mduma na Bi. Eva Valerian – Washington DC
Imetolewa
na
Ingiahedi
Msemaji wa
Wizara ya fedha.


Post a Comment