Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania-TCAA yafanya mkutano wa mwaka mkoani Arusha



DSC01706
 
Viongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)akiwemo mkurugenzi wake Fadhil Manongi wakimkaribisha Mgeni Rasmi Kaimu Mkuu wa Arusha na ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa wakati alipowasili kufungua rasmi baraza la tatu la wafanyakazi TCAA lililofanyika katika hoteli ya Naura Springs Hotel, jijini Arusha (April 11-12,2013)(Picha na Mahmoud Ahmad Arusha)
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Mahmoud Ahmad Arusha
Mamlaka ya usafirishaji wa Angani (TCAA)imetakiwa kukabiliana na changamoto ya usafirishaji wa mizigo iendayo nchi za nje ikiwemo mizigo ya maua kwani imekuwa ikiikosesha serekali mapato japo kumekuwapo na changamoto mbali mbali kwenye usafirishaji wa mizigo hapa nchini.


Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mullongo kwa niaba yake namkuu wa wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa wakati akifungua mkutano wa mwaka wa mamlaka hiyo jijini hapa na kuitaka mamlaka hiyo kukabiliana na changamoto hiyo ya ukosefu wa ndege za mizigo.
Munasa alisema kuwausafirishaji wa mizigo kwenye usafiri wa anga umekuwa na changamoto licha ya mizigo kuwa mingi hivyo mnawajibu wa kutafuta usafiri wa mizigo kama mlivyofanya kwenye usafiri wa abiria na kupata mafanikio kwa muda mfupi.
“Mnawajibu wa kushughulikia usafiri wa mizigo kama mlivyoshughulikia usafirishaji wa abiria humu nchini kwani sekta mbal;I mbali zimakuwa na bidhaa mbali mbali zinazohitaji kupelekwa sokoni kwa wakati”alisema munasa
Kwa upande wake mkurugenzi wa mamlaka ya usafirishaji wa Anga Fadhili Manongi alisema kuwa shirika hilo limepata mafanikio kwenye usafirishaji abiria kutoka 2milion hadi milion4 humu nchini likiwa ni ongezeko la asilimia 90% kwenye miaka ya2005 hadi sasa huku akisema kuwa abiria kwenye viwanja vya Arusha na kia wameongezeka kutoka 360,331 hadi kufikia 715,356 ni dhahiri mkoa huu umechangia kwenye ongezeko hili la abiria hapa nchini.
Alisema kuwa hiyo ni sawa na asilimia 98% ya abiria waliosafiri kwenye viwanja hivyo huku mashirika ya kimataifa yakiongezeka kutoka 12 hadi kufikia 17 huku safari za kimataifa zikiongezeka kutoka87 hadi 209 katika kipindi hicho huku akisema kuwa serekali inaendelea kukiuza kiwanja cha Kilimanjaro ili mashirika mbali mbali ya kimataifa yalete ndege zake uwanjani hapo.
Manongi alisema kuwa hawajafaniwa kuzileta ndege za mizigo kwenye uwanjao huo wa Kia iliziweze kubeba maua na mizigo mingine ya kilimo yanayotakiwa kwenye soko la nje kwani bidhaa nyingi zimekuwa zikisafirishwa kwa njia ya barabara kwenda jwenye uwanja wa Jomo Kenyatta nchi ya jirani hivyo wameandaa juhudi za maksudi kufanikisha kuzileta ndege za mizigo uwanjani hapo kukabiliana na ushindani huo.
“Tatizo hapa ni kuwa ndege nyingi zinakuwa hazina mzigo wakutosha kuleta hapa nchini wakati ndege hizo zinamzigo wa kuchuwa kwenye uwanja huo hii ndio changamoto lakini tutaifanyia kazi’’alisema Manongi.

credits: Fullshangwe
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top