Mbunge wa
Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), kiakabidhi mifuko ya saruji kwa
viongozi wa Kata ya Kiomoni.
Na
Mwandishi Wetu, Tanga
MBUNGE wa
Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), awametaka wananchi wa mkoa wake
kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika maeneo
yao.
Kauli hiyo
aliitoa kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza katika ziara yake hiyo katika
kata za halmashauri ya jiji la Tanga na Wilaya ya Pangani, ambapo alisema ni
muhimu kwa kila mwanajamii kutambua wajibu wake.
“Suala la
amaendeleo halina itikadi na sasa sio wakati wa kampeni za uchaguzi, ni jukumu
letu kwa viongozi wa Mkoa wa Tanga, kuhakikisha tunashiriki katika miradi ya
maendeleo kwa dhati.
“Ni wazi
Mkoa wa Tanga tuna kila sababu ya kuhakikisha tunaimarisha uchumi wetu hasa
baada ya miaka kadhaa viwanda vyake kufa kutokana na kutokuwepo na usimamizi
mzuri. Ikiwa kila mtu atatambua wajibu wake ni wazi tutafanikiwa kufikia lengo
letu,” alisema Mwidau.
Alisema
kutokana na hali hiyo kila mara amekuwa akishiriki katika kuhamasisha maendeleo
katika maeneo yote ya mkoa huo bila kujali uongozi wa kaa upo chini ya chama cha
CUF au CCM.
“Tanga
tuna ardhi nzuri na tuna kila sababu ya kujivunia jambo hili ingawa kukosekana
kwa usimamizi madhubuti kwetu imekuwa ni kilio kikubwa kwa wananchi wetu
tunaowaongoza, wabunge wote wa mkoa huu tuna wajibu wa kuliangalia hili,”
alisema Mbunge Mwidau.
Katika
ziara hiyo akiwa wilayani Pangani Mwidau, alisema kuwa amefurahishwa kuona
wananchi na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwera kuamua kuchimba kisima
kikubwa zaidi ya kilichopo sasa na katika hilo amefurahishwa kuona mchango wa
awali wa mashine aliyoitoa imewezesha kujengwa kwa kisima kisima kingine kikubwa
cha futi 45 na kipenyo cha nchi sita.
Post a Comment