Afisa Muuguzi wa Kituo cha Afya cha 'Town' mkoani
Lindi, Assumpta Mpiri, akimtoa damu mtoto mchanga kupitia kisigino, tayari kwa
kuikausha na kuipeleka maabara kuu ya Taifa ya Muhimbili kwa njia ya mashine
'sms printer' ambayo pia katika kipindi kifupi inauwezo wa kupokea majibu ya
vipimo hivyo tayari kwa kumkabidhi mzazi wa mtoto huyo. Mashine hizo takribani 8
zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu 11, zimetolewa mkoani humo kwa
msaada wa Vodacom Foundation chini ya uratibu wa Taasisi inayojishughulisha na
Mpango wa Tafiti zinazohusiana na Afya ya Uzazi ya EGPAF
Afisa Muuguzi wa Kituo cha Afya cha 'Town' mkoani
Lindi, Faida Ibrahim, kwa kushirikiana na Meneja wa Vodacom Foundation, Grace
Lyon, akimtoa damu mtoto mchanga kupitia kisigino, tayari kwa kuikausha na
kuipeleka maabara kuu ya Taifa ya Muhimbili kwa njia ya mashine ya kisasa 'sms
printer' ambayo pia katika kipindi kifupi inauwezo wa kupokea majibu ya vipimo
hivyo tayari kwa kumkabidhi mzazi. Mashine hizo takribani 8 zenye thamani ya
zaidi ya Dola za Marekani elfu 11, zimetolewa mkoani humo na Vodacom Foundation,
chini ya uratibu wa Taasisi inayojishughulisha na Mpango wa Tafiti zinazohusiana
na Afya ya Uzazi ya EGPAF
Mratibu wa Uchunguzi wa VVU kwa Watoto Wachanga kutoka
Taasisi Tafiti za maendeleo ya Afya ya Uzazi wa mtoto, baba na mama wa EGPAF,
Georgiah Kasori (katikati) akitoa maelekezo ya namna bora ya kutumia mashine za
kisasa 'sms printers' zinazowezesha upatikanaji wa haraka wa vipimo vya VVU kwa
watoto wa umri wa kati ya mwezi 1 hadi miezi 18 kwenye Zahanati ya 'Town' katika
ziara iliyofanywa na Maofisa wa Vodacom Foundation kukagua ufanisi wa mashine
hizo mkoani Lindi. Zahanati hiyo ni miongoni mwa Vituo vya Afya vilivyonufaika
na mashine hizo takribani 8 zilizotolewa kwa hisani ya Vodacom
Foundation
Mtaalamu wa Maabara ya Hospitali ya Mkoa wa Lindi,
Julius Mwansimba, (kulia) akimuonesha Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon,
ufanisi wa mashine 'sms printers' zinazowezesha upatikanaji wa haraka wa majibu
ya vipimo vya VVU kwa watoto wachanga ndani ya maabara ya hospitali hiyo jana.
Vodacom Foundation chini ya uratibu wa Taasisi inayojishughulisha na Tafiti za
Afya ya Uzazi wa mtoto, baba na mama ya EGPAF hivi karibuni ilitoa msaada wa
mashine hizo zipatazo 8 mkoani Lindi, zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani
elfu 10
Afisa Muuguzi wa Hospitali ya mkoa wa Lindi, Zainab
Mathradas, (kulia), akimkabidhi mmoja wa wadau wa huduma za afya, ambaye ni
Meneja wa Vodacom Foundation, Grace Lyon, taarifa ya takwimu na matokeo ya
ufanisi wa huduma ya Afya ya Uzazi wa mtoto, baba na mama mkoani Lindi. Wengine
wanaoshuhudia ni Maafisa waandamizi kutoka Taasisi inayojishughulisha na Mpango
wa Tafiti zinazohusiana na Afya ya Uzazi ya EGPAF. Vodacom Foundation hivi
karibuni ilichangia mashine 8 'sms printers' zenye gharama ya zaidi ya Dola
Marekani elfu 10 mkoani Lindi, zinazowezesha upatikanaji wa haraka wa majibu ya
vipimo vya VVU kwa watoto wachanga.
Mkazi wa Matokeni mkoani Lindi, ambaye anaishi na
Virusi vya Ukimwi, Iman Bakari, akiwaeleza wanahabari, na maofisa kutoka Vodacom
Foundation na Taasisi inayojishughulisha na Afya ya uzazi wa mtoto, baba na mama
ya EGPAF, namna mashine za kisasa 'sms printers'zilivyomuwezesha kupata majibu
ya vipimo vya VVU vya watoto wake wawili kwa urahisi na haraka. Mashine hizo
takribani 8 zenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani elfu 10, zimetolewa
mkoani humo na Vodacom Foundation, chini ya uratibu wa Taasisi
inayojishughulisha na Mpango wa Tafiti zinazohusiana na Afya ya Uzazi ya EGPAF
.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Lindi, Dk Sonda Shaaban,
akifafanua jambo mbele ya maofisa wa Vodacom Foundation na Taasisi
inayojishughulisha na tafiti zinazohusiana na Afya ya Uzazi ya EGPAF, (hawapo
pichani), sanjari na kutoa tathmini ya jinsi mkoa huo ulivyojipanga kukabiliana
na changamoto ya afya ya Uzazi wa mtoto, baba, na mama kwenye eneo la maambukizi
mapya ya VVU toka kwa baba na mama kwenda kwa mtoto. Vodacom Foundation hivi
karibuni ilichangia mashine 8 za kisasa 'SMS PRINTER' zenye thamani ya zaidi ya
Dola za Marekani elfu 10 ndani ya mkoa huo, katika kuwezesha upatikanaji wa
haraka wa majibu ya vipimo vya VVU kwa watoto wachanga.
Post a Comment