Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mkuu wa mkoa wa Singida acharuka na kumtaka diwani wa kata ya Ipembe kuachia ngazi huku akimsifu mbunge wa Singida mjini Mh. Mohammed Dewji.

 

Mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi akitoa taarifa yake ya utekelezaji wa ilani cha uchaguzi ya CCM kwa mkuu wa mkoa wa Singida (aliyeketi) Dk.Parseko Kone. Dk.Kone alifanya ziara ya kiazi katika manispaa ya Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Paresko Kone akizungumza na wakuu wa idara wa manispaa ya Singida na halmashauri ya wilaya ya Singida kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Singida.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Singida na manispaa ya Singida wakifuatilia kwa makini taarifa iliyokuwa ikitolewa na mkuu wa wilaya ya Singida, kwa mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone alihutubia wananchi wa kata ya Mandewa manispaa ya Singida ikiwa ni sehemu yake ya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye manispaa ya Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida. Dk.Parseko Kone (kulia aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo kwa diwani wa kata ya Mitunduruni Pantaleo Sorongai (wa kwanza kushoto) juu wa ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara katika shule ya sekondari ya Mitunduruni.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Mandewa waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone kuzungumza na wananchi.
Baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule ya sekondari yaliyojengwa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mohammed Dewji kutoka kwenye mfuko wake binafsi.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mkuu wa mkoa wa Singia Dkt. Parseko Vicent Kone amezitaka kamati za ujenzi wa maabara katika shule za sekondari, kuongeza juhudi kukamilisha ujenzi huo ili kuwavutia wafadhili/wahisani kutoa michango mbalimbali ikiwemo ya vifaa vya maabara.
Dk.Kone ametoa wito huo kwa nyakati tofauti wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu kwa kila shule za sekondari 17 za manispaa ya Singida.
Amesema uzoefu unaonyesha wazi kwamba wafadhili/wahisani au watu wenye uwezo kiuchumi, huvutiwa zaidi au kirahisi kuchangia miradi ya maendeleo, baada ya kuona juhudi za wananchi kwenye mradi husika.
“Ninyi wakazi wa jimbo la Singida mjini, mna bahati kubwa sana.
Mbunge wenu Mh. Mohammed Dewji ni mbunge mzuri ambaye ni msikivu na ana moyo wa dhati wa kusaidiana na wananchi wake katika kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo.Msaidieni kwa kujenga vyumba vya maabara na yeye nina imani atamalizia mambo ambayo yatakuwa juu ya uwezo wenu”,amesema Dk.Kone.
Katika ziara yake Dkt. Kone ameonyesha dhahiri kutokufurahishwa na kitendo cha baadhi ya shule za sekondari kuanza kuchimba misingi ya vyumba vya maabara siku chache kabla ya ziara yake ya kikazi kuanza.
Moja ya shule hizo ni ile ya kata ya Ipembe iliyopo jirani na shule ya msingi Kibaoni ambayo diwani wa kata hiyo ni Twalib Kihara.
Dkt. Kone alimuuliza diwani Kihara ni lini ujenzi wa chumba cha maabara utafikia hatua ya lenta.
Kihara baada ya kukaa kimya kwa sekunde kadhaa, alijibu,”mkuu hatua ya lenta tutaifikia Juni mwishoni mwaka huu.
Dkt. Kone alimwambia “hatuwezi kukuruhusu ufanye unavyotaka wewe, tunakuagiza hadi Mei 25 mwaka huu, jengo liwe limefikia kwenye hatua ya lenta na kama huwezi, achia ngazi, je utaweza au huwezi?”.
Kihara,alijibu “ndio mkuu nitaweza na ukija Mei 25 mwaka huu, utakuta ujenzi umefikia hatua ya lenta”
MO BLOG
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top