MKUU WA WILAYA YA KAHAMA BENSON MPESYA
AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WALIOHUDHURIA KATIKA MSIBA HUO.
KAHAMA
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mh.Benson Mpesya ameliagiza jeshi la Polisi wilayani humo
kuhakikisha ndani ya wiki moja wanawatia
mbaroni watu waliofanya mauaji ya Sajenti Salim Mtepa (41) usiku wa kuamkia
leo.
Agizo
hilo amelitoa leo wakati akitoa salamu za pole nyumbani kwa marehemu ambapo
mwili wa marehemu ulikuwa ukiagwa kabla ya safari ya kuelekea jijini Dar es
salaam.
Sambamba
na hayo amewataka vijana wilayani kahama kutafuta pesa kwa njia zilizo halali na
kuacha kutafuta pesa kwa njia za mkato ikiwemo wizi,ukabaji na
utapeli.
Katika
hatua nyingine amewataka vijana wasiokuwa na ajira mjini kurudi vijijini kwao
ili kujishughulisha na kilimo wakiwasaidia wazazi wao badala ya kukaa vijiweni
na kujiingiza katika makundi mabaya.
Kwa
upande wake Mkuu wa kituo cha Polisi wilayani Kahama George Simba amemwambia
mkuu wa wilaya kuwa tayari zoezi la kuwasaka watu hao limeanza na kuongeza kuwa
lazima watu hao wapatikane.
Naye
Kaimu kamanda mkuu wa Mkoa Wa Shinyanga Onesmo Lyanga amesema kuwa damu ya
Sajenti Salim haiwezi kwenda bure na kwamba watahakikisha jeshi la Polisi
linawatia mbaroni watuhumiwa hao.
Pamoja
na hayo ametoa wito kwa Wananchi wilayani kahama kutoa taarifa za siri endapo
watapata tetesi zozote kuhusu tukio hilo.
kb blog


Post a Comment