
MBUNGE
Viti Maalumu, Susan Kiwanga (CHADEMA), na ujumbe wa benki ya NMB Kanda
ya Mashariki, wamenusurika kuvamiwa na watu wanne wanaosadikiwa kuwa
majambazi katika kijiji cha Mbingu wilayani hapa.
Kunusurika
huko kulikotokana na wasamaria wema kuwashtukia watua hao majira ya saa
8 mchana na kutoa taarifa kituo cha polisi Mbingu waliofanikisha
kuwanasa kabla viongozi hao waliokuwa shule ya msingi Mtyangimbole iliyo
kijiji cha Ikule na shule ya msingi Kitete, iliyo kijiji cha
Mkangawalo, kata ya Mngeta, kutoa msaada wa madawati 78.
Mbele
ya mbunge Susan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Morogoro
aliyeamua kupita kituoni hapo kuwashuhudia watu hao, Mkuu wa Kituo cha
Polisi Mbingu, Adriano Mayo, aliwataja waliokamatwa kuwa ni Shomari
Miraji (29) mkazi wa Kibaha Mwendapole, Shukuru Bakari (33), mkazi wa
Mlandizi, Abdalah Ally (33), mkazi wa Dar esSalaam na Stumai Shaban (30) mkazi wa Bagamoyo.
“Baada ya mahojiano walikiri kuwa kuna baadhi ya matukio waliyafanya,” alisema polisi huyo.
Hata
hivyo, Mayo alimwambia mbunge huyo kuwa kituo hicho hakina jengo la
kuhifadhia wahalifu, ofisi, silaha, vifaa vya usafiri kama gari kwa
ajili ya doria katika barabara hiyo na fedha za hamasa juu ya
upatikanaji taarifa za kihalifu.
Mbali na
mkuu huyo wa kituo kutoa malalamiko na adha dhidi ya uduni wa mazingira
ya kazi, ofisa mtendaji wa kijiji hicho Salum Sadala alimwomba mbunge
huyo kukisaidia kijiji hicho upatikanaji wa fedha shilingi mil.6
kukamilisha jengo la kituo hicho cha polisi kijijini hapo ambalo liko
katika hatua ya mwisho ya ujenzi naye Susan aliahidi shilingi 200,000
mwezi ujao.
“Mbunge
tumekwama kukamilisha jengo hili na kituo cha polisi ili tuimarishe
usalama; ni kiasi kisichozidi shilingi mil.6 tunahitaji; tunaomba popote
ufikapo tusaidie kupata mfadhili maana hali ya sasa kwa wananchi si
nzuri kuwabana michango,” alisema Sadala.
chanzo: Tanzania Daima
Post a Comment