Wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida imetangaza ‘operation ondoa tembe’baada ya matukio ya wakazi wake kuendelea kupoteza maisha kutokana na kuangukiwa na nyumba za tembe. Wilaya hiyo mpya imeagiza kila mkazi awe na nyumba bora kama njia mojawapo ya kukomesha vifo vinavyotokana na kuangukiwa na nyumba za tembe.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Mvua ya kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Singida zimesababisha watu wanne wakazi wa wilaya ya Mkalama na mifugo 14 ya aina mbalimbali kufariki dunia baada kuangukiwa na nyumba za tembe.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Hezroni Msule wakati akizungumzia madhara/hasara mbalimbali zinazosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Msule alisema kuwa kwa sasa bado hawajapata majina ya wakazi hao wa wilaya ya Mkalama waliofariki dunia baada ya kuangukiwa na nyumba za tembe.
Amesema kuwa pamoja na vifo hivyo vya watu pamoja na mifugo, pia mvua hizo zimeleta uharibifu mkubwa wa zaidi ya ekari 1,119 za mazao mbali mbali na kuangusha nyumba za tembe 543 na za bati 171.
Akifafanua zaid Msule amesema maafa hayo yametokea katika kipindi cha wiki moja ya kwanza ya mwezi huu wa nne.
Msule amesema kuwa idadi kamili ya watu waliokosa mahali pakuishi na hasara iliyopatikana bado haijafahamika
.Kazi ikikamilika ya kukusanya taarifa zaidi ya kujua idadi ya watu hao waliokosa makazi na hasara iliyopatikana, taarifa zitatolewa ili kuijulisha jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda amesema ili kukabiliana na athari za watu kupoteza maisha yao kutokana na kuangukiwa na nyumba, kuanzia sasa wilaya za Iramba na Mkalama zimeanzisha operesheni maalumu inayojulikana kwa jina la ‘ujenzi wa nyumba za tembe’.
Nawanda ambaye pia ni kaimu mkuu wa wilaya ya Mkalama amesema ofisi yake inafanya mawasiliano na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi ili kusogeza karibu vifaa vya ujenzi kwa wananchi waweze kujijengea nyumba bora.




Post a Comment