Mkuu wa kitengo cha Masoko
na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa(katikati)akiongea na Mshindi
wa Droo ya mwishi ya "MAHELA "Bw.Valelian Nickodemus(22) wa Mkoa wa Kigoma
aliyejishindia shilingi Milioni 100.kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya
kubahatisha nchini Bw.Mrisho Milau na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa
Vodacom Tanzania,Bw. Benjamin Michael.
Kutoka kushoto,Msimamizi wa
Michezo ya kubahatisha nchini Bw.Mrisho Milau,Meneja Uhusiano wa Vodacom
Tanzania Bw.Matina Nkurlu,pamoja na Meneja wa Huduma za ziada wa kampuni hiyo,
Bw. Benjamin Michael,wakichezesha droo ya mwisho ya "MAHELA"ambapo Bw.Valelian
Nickodemus(22)Mwanafunzi wa Chuo cha uwalimu Mkoani Kigoma alijishindia kitita
cha shilingi Milioni 100,kupitia promosheni hiyo.
Mkuu wa kitengo cha Masoko
na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa(katikati)akizungumza na
waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kumpata mshindi wa Droo ya
mwishi ya "MAHELA "Bw.Valelian Nickodemus(22) wa Mkoa wa Kigoma aliyejishindia
shilingi Milioni 100.kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini
Bw.Mrisho Mlau na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.
Benjamin Michael.
Hatimaye Mshindi wa Milioni
100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela amepatikana ikishuhudia Mwanafunzi chuo cha
Ualimu cha Mkoani Kigoma Bw.Valelian Nickodemus(22) akiibuka mshindi kupitia
droo kubwa iliyochezeshwa leo jumatatu.
Mshindi huyo amepatikana
miongoni mwa mamilioni ya washiriki walioshiriki kucheza katika promosheni hiyo,
Katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya simu Mshindi huyo ameishukuru kampuni
ya Vodacom kwa kumuwezesha kushinda kiasi hiko kwani hayakuwa mategemeo yake
katika maisha yake.
"Watu wengi hawakuwa
wanaamini kuwa Promosheni hizi ni za kweli, Sikuwa na pesa ya kucheza moja kwa
moja katika Promosheni hii ila nilipotumiwa pesa ya matumizi na mzee niliamua
kuweka na kushiriki katika Promosheni hii, Hakika nimefurahi sana na
ninawashukuru Vodacom, alisema Nickodemus.
Kwa upande wake mkuu wa
kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa
amewapongeza Wateja wa mtandao huo kwa kushiriki katika promosheni hiyo na
kumpongeza kwa upekee mshindi wa Promosheni hiyo na kujinasibu kuwa anajivunia
mafanikio ambayo Promosheni hiyo imeyapata kwa kufanikiwa kubadili maisha ya
mamia ya Watanzania.
"Sisi kama Vodacom
tumefurahi kwa kumpata mshindi wetu wa mwisho ambaye ameibuka kidedea kati ya
Mamilioni ya Watanzania lazima tukiri kuwa ni bahati kubwa na tunatoa pongezi za
kipekee kwa mshindi wetu, alisema Twissa na kuongeza kuwa "Zaidi ya yote
tunajivunia kwa upekee kabisa namna ambavyo promosheni hii imebadilisha mamia ya
maisha ya Watanzania, Tumepata washindi kutoka katika Nyanja mbalimbali wakiwemo
wakulima, wafanya biashara ndogondogo wanafunzi pamoja na wastaafu wengi ambao
nao wameendelea kuboresha maisha yao.
Tangu Promosheni ya MAHELA
kuzinduliwa tarehe 24 Mwezi wa kwanza na washindi 333 wamepatikana na kushuhudia
kiasi cha Shilingi milioni 480 zikitolewa hadi sasa.
Post a Comment