Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi Juliet Rugeiyamu
Kairuki kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC).
Taarifa iliyotolewa jana,
Jumatatu, 22 Aprili, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK)
Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Aprili 12, mwaka huu,
2013.
Bibi Kairuki ni Mwanasheria
mwenye Shahada ya Kwanza na ya Uzamili kwenye sheria. Ni mtaalam wa miradi ya
ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private
Partnership). Kati ya mwaka 2002 na 2008 alikuwa Meneja wa Mradi
wa Public Private Partnership Capacity Building in SADC, katika Chama
cha Mabenki ya Afrika Kusini (The Banking Association South Africa).
Kuanzia mwaka 2008 hadi sasa Bibi Kairuki ni Meneja Mkuu wa Idara ya Benki na
Huduma za Fedha katika taasisi hiyo.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu.
DAR ES
SALAAM.
22 Aprili,
2013



Post a Comment