|
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbasi Kandoro akizungumzana waandishi wa habari
ofisini kwake amesema Raisi Kikwete anatalajiwa kuwasiri mkoani hapa
Apri 30 mwaka kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa songwe majira ya
saa4 na Nusu asubuhi. |
|
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Mbeya wakimsikiliza mkuu wa mkoa Mbeya |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk
Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za siku ya
wafanyakazi duniani Mei mosi itakayofanyika kitaifa Mkoani Mbeya.
Pamoja na kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo
pia anatarajiwa kuzungumza na wakuu wa shule na Wamiliki wa Vyuo binafsi (
katika ukumbi wa mkapa Apri 30 mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbasi Kandoro
akizungumzana waandishi wa habari ofisini kwake amesema Raisi Kikwete anatalajiwa
kuwasiri mkoani hapa Apri 30 mwaka kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa
songwe majira ya saa4 na Nusu asubuhi.
Amesema mara baada ya kuwasili mkoani hapa
atazungumza na wamiliki wa shule hizo ambao alitajiwa kuzungumza nao Aprii 29
mwaka lakini ikashindikana kutokana na kuwepo kwa mkutano wa viongozi nchi za
Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.
Amesema mara baada ya kuingiliana kwa ratiba
hiyo baadhi ya ratiba ambazo zilitarajiwa kufuatwa zimevunjwa hasa zile za
uzinduaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo hasa katika Wilaya ya
Rungwe,Mbarali,Mbozi ambapo Mweshimiwa Rais Kikwete anatalajiwa kufanya ziara nyingine
kwa ajili ya shuhuli hizo hapo baadae.
Kutokana na hali hiyo Mkuu huyo wa Mkoa amesema
mara baada ya kuzungumza na wakuu wa shule pamoja na viongozi wa chama cha
wafanyakazi( Tucta)ambapo baada ya hapo atapokea taarifa ya mkoa pia kuwa
mgeni rasmi kwenye kilele cha Mei mosi ambapo jioni atalejea jijini Dar es
salaam kuendelea na vikao vingine.
Pia katika taarifa yake kwa waandishi wa habari
jijini hapa Kandoro amewaomba radhi wananchi wa mkoa wa mbeya ambao walijiaanda
kwa lengo la kumpkea kiongozi wao kutokana na kusitishwa kwa tatiba hizo.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa wa Mkoa wa mbeya
Ndugu Abbasi Kandoro amewataka wananchi wa jiji hilo la mbeya kujitokeza kwa
wingi kumraki Mheshimiwa Rais mara atakapo wasiri jijini Mbeya katika uwanja wa
kimataifa wa Sonwge( SIA) pamoja na kujitokeza kwa wingi katika sherehe za
Meimosi kitaifa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa.
|
on Tuesday, April 30, 2013
Post a Comment