Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akichanganya udongo wa Tanganyika na zanzibar kuashiria Muungano wa nchi hizi mbili mnamo aprili 26 mwaka 1964
Ndugu Wa
Tanzania,
Kwa niaba ya tawi la Chama
Cha Mapinduzi Uingerez,na kwa niaba yangu binafsi, Napenda kutoa salamu kwa
Mwenyekitiwa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania,na kwa Watanzania wote kwa ujumla kwa kutimiza miaka 49 ya Muungano
wa nchi yetu, TANZANIA.
Pamoja na salamu hizo,
binafsi na kwa niaba ya wana CCM UK ,napenda kuwaomba na kuwakumbusha WaTanzania
wenzangu, tuendelee kuuenzi na kuulinda Muungano wetu kwa kudumisha AMANI,
UPENDO, UMOJA, UTULIVU na MSHIKAMANO. Hizi ndizo silaha zilizoweza kuulinda
Muungano huu ambao umetuletea Heshima ya kipekee Duniani kote, kwa nusu karne
sasa.
Ndugu Wa Tanzania,
nawasihi kamwe tusichezee amani tuliyonayo. Tujifunze kutoka nchi mbalimbali
duniani ambazo wamechezea amani yao na sasa wamo ndani ya dimbwi kubwa la
machafuko, mauaji ya halaiki na yanayoendelea kila
kukicha
Aidha, Watanzania wa Nje ya
Nchi (Diaspora)tunajivunia na kutambua kwamba tuna nafasi ya pekee ya kuchangia
katika maendeleo ya Nchi yetu Tanzania katika Nyanja tofauti . Mojawapo ya
Mchango wetu Mkubwa kwa Taifa ni kufuatilia kwa ukaribu mambo yanayoendelea
nyumbani ,na kutoa mchango wetu wa kimawazo pale
inapobidi.
CCM-UK tutaendelea kutoa
shukrani za dhati kwa Mwenyekitiwa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete , pamoja na Serikali yake anayoiongoza kwa
kuona umuhimu wa kutushirikisha Wana Diaspora na kuthamini mchango
wetu.
Tunafarijika sana na
kuahidi siku zote kwamba tutaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya
Tanzania, kama inavyowezekana kwa raia wengine
Wengi Ulimwenguni wanaoishi
nje ya Nchi zao na wana changia kukuza uchumi na kuendeleza jamii zao kwa
kutumia ujuzi na ufanisi waliojifunza ughaibuni.
Mwisho nawatakieni
watanzania wenzangu kusherehekea sikukuu ya muungano kwa amani na Utulivu
mkubwa.
Tuwaenzi waasisi wetu, Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Aman Karume kwa kuulinda
muungano.
MAISHA BORA KWA KILA
MTANZANIA, SI NDOTO YANAWEZEKANA.
Kwan niaba ya CCM UK –
Nawatakia Watanzania wote popote pale walipo Duniani Maadhimisho na Sherehe
njema za siku hii adhimu.
MUNGU IBARIKI AFRIKA –
MUNGU IBARIKI TANZANIA
KIDUMU CHAMA CHA
MAPINDUZI.
—————————————————–
Mariam A.
Mungula
KATIBU
CHAMA CHA MAPINDUZI –
UINGEREZA
Post a Comment