Aliyekuwa
mjumbe baadae katibu mkuu wa CHANETA Anna Kibira amechaguliwa tena kuwa
mwenyekiti wa chama cha mpira wa pete chaneta Katika uchaguzi uliofanyika jioni
ya leo hii Mkoani Dodoma , huku msimazi wa uchaguzi huo akiwa mkuu wa wilaya ya
bahi na aliyekuwa Mtangazaji wa zamani wa itv Betty Mkwasa .
Anna Kibira
amemshinda mpinzani wake Shy-Rose Bhanji kwa tofauti ya la kura arobaini
katika nafasi ya uenyekiti Anna Kibira amepata kura 61 dhidi ya mpinzani wake
Shy-Rose Bhanji ambaye amepata kura arobaini na moja .
Aidha
kulikuwa na nafasi mbalimbali ambazo zilikuwa zikigombewa katika chama hicho cha
mpira wa pete ambapo kulikuwa na wajumbe wa kamati ya utendaji ambao
walikuwa wagombea tisa lakini
wamepataikana wagombea sita tu.
Grace Khatib
ambaye alikuwa hana mpinzani katika nafasi ya mweka hazina alipata kura za ndio
66 na kura za hapana 16 kati ya kura 82 zilizopigwa.
Katika
nafasi ya makamu mwenyekiti kulikuwa na wagombea wawili Zainab Mbiro na Agnes
Madasila katika nafasi hiyo Zainabu Mbiro alipata kura hamsini saba wakati
mpinzani wake amepata kura 27
Kwa maana
hii CHANETA imepata safu mpya kabisa ya uongozi baada ya ile ya mwanzo ile
kuamua kuachia ngazi na wagombea wengine kuamua kutokugombea kabisa uongozi
katika chama hicho cha mchezo wa pete kwani safu mpya inatakiwa kufanya kazi ya
ziada kufikia malengo ya kuinua mchezo wa mpira wa pete kwani uongozi uliopita
uliiwezesha CHANETA kuifikisha timu ya taifa ya mchezo huo katika mashindano ya
dunia.
Chama
kiliweza kuaandaa michuano ya mataifa ya afrika ni wazi kabisa wanachangamoto
kubwa ya kufanya japokuwa mara baada ya ushindi kibira amesema kuwa anataka
kuupeleka mchezo huo mikoani na kwenda kuuimarisha zaidi
vijijini .



Post a Comment