Kamanda wa polisi Mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimek akizishika nyara za serikali hizo ambazo zimekamatwa(mikia ya tembo) Kwa hisani ya http://demashonews.blogspot.com
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma katika wilaya ya Tunduru kijiji cha Mbalikiwa kata ya Ligunga tarafa ya Matemanga linamshikilia kijana ambaye anafahamika kwa jina la Bakari Said mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mkazi wa eneo hilo kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali.
Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Deusidedit Nsimeki ameyasema hayo jana mapema wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema jumla ya mikia ya Tembo 10 imekamatwa na askari ambao walikuwa doria katika eneo la Mbalikiwa Febriari 5/2013 majira ya saa:7 usiku, jumla ya idadi hiyo ya mikia ni sawa na idadi ya Tembo 10 waliouwawa na idadi ya meno ni 20 yenye jumla ya dola za kimarekani elfu 15 sawa na zaidi ya milioni 245 kwa fedha za kitanzania
Mtuhumiwa Bakari Said jana amefikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara haramu ya nyara za serikali ambapo taarifa za tukio hilo la uhalifu zilipatikana kutoka kwa raia wema pia kamanda wa polisi aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wao wa dhati hili kwa jeshi la polisi ili kuweza kudhibiti kabisa huarifu huo.
Nyara za serikali hizo ambazo zimekamatwa
Post a Comment