Na
Bryceson Mathias,
SHILINGI
80,000/- Elfu zikiwa ni gharama za Matofali 800 (kila moja Sh. 100/-), na Sh.
45,000/- zikiwa ni michango ya wana kijiji wa Mafuta, ndizo zilizoelezwa kuwa
kigezo cha kumuengua Uenyekiti wa Serikali ya Kijiji Bw. Waziri Juma toka mwaka
jana.
Hayo
yamebainika jana baada ya Mwandishi wa Habari hizi kufuatilia kujua nini
kinacholeta vurugu na Migogoro ndani ya Serikali ya kijiji hicho ambapo sasa
wananchi wanatishia kukataa kufanya kazi zote na Mtendaji Kata ya Mhonda Bw.
Emili Mjenja.
Akizungumzia Mtafaruku huo Mjumbe wa Halmashauri ya
Kijiji Bw. Jafari Seleman mjumbe alikiri kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi
kati yaa baadhi ya Viongozi wa Kata na wale wa kijiji hicho ambapo alisema,
kumekuwa hakuna Ueledi katika Mapato na matumizi ya Michango yao.
“Si jambo
la Siri kumekuwa hakuna mahusiano mema kati ya Viongozi wa Kata na wananchi wa
Kijiji cha Mafuta, ambapo wanasema viongozi wa kijiji wanashirikiana na wa Kata
kwa namna fulani, kuhujumu Mali, Michango na Mapato ya Kijiji, ndio maana
wamemkataa Mwenyekiti”. Alisema Selemani.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa sasa Bw. Nicholous Mbelwa aliyechaguliwa na wananchi baada ya
kuangushwa Bw. Juma aliwalaum viongozi wa Kata akiwatuhumu kuwa wanafanya mchezo
na Masha ya Wananchi ambao wanateseka kuokoa kuokoa nguvu na juhudi za
serikali.
Aidha
Diwani wa Kata ya Mhonda Bw. Salum Mzugi (CCM) alipoongea na mwandishi wa habari
hizi alisema, anasikitishwa kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara inayohusu
upinzani wa vyama kwa sababu inawaondolea wananchi maendeleo waliokusudia,
ambapo aliahidi kuyapatia ufumbuzi wa kina.
Kiti cha
mwenyekiti wa Kijiji hicho, kimekuwa na Mvutano toka mwaka jana Julai 7, 2012,
ambapo wanakijiji walimng’oa Mwenyekiti Juma kwa tuhuma za ubadhirifu na madai
ya kukwamisha maendeleo ya wananchi, ambapo Mtendaji Kata Bw. Mjenja anatetea
asiendelee, huku wananchi wakipinga.
Credits: Habari Mseto Blog
Post a Comment