Crane (yenye rangi ya njano) ya shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA) ambayo ilikuwa inainua mabehewa yaliyopata ajali ikijaribu kuinuliwa na Crane nyingine ya Shirika hilo jana jioni katika eneo la Mzenga Kisarawe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi akitoa Malekezo kwa Uongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA),jana jioni alipotembelea eneo hilo ambapo crane iliyokuwa inanyanyua mabehewa yaliyoanguka ilipata ajali ya kuangukia mwishoni mwa wiki hii katika neon la Mzenga Kisarawe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, (Mwenye tai nyeusi), akimsikiliza Meneja wa Usalama wa TAZARA, Bw. Elisha Mhoka, wakati akitoa maelezo ya namna ambavyo Crane hiyo ilianguka na njia zinazotumika kuhakikisha inasimama. Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu walitembelea eneo hilo jana jioni kuangalia kasi ya kuisimamisha crane iliyoanguka aidha Katibu Mkuu huyo ameiagiza TAZARA kuhakikisha kazi hiyo inakamilika haraka iwezekanavyo.
Crane inayosaidia kuiinua Crane iliyoanguka mwishoni mwa wiki wakati ikijaribu kuinua mabehewa yaliyopata ajali katika eneo la Mzenga Kisarawe kama yalivyokutwa jana jioni,wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi