Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

VIONGOZI WENGI CHADEMA WANAGANGA NJAA....NAPE NNAUYE


Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye amesema Chadema ni chama kilichovamiwa na watu wanaotumia siasa kuganga njaa.Nape alisema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

“Ndugu zangu kuweni macho kwa sasa, siasa imeingiliwa na watu wasiokuwa na sifa za uongozi na kazi yao kubwa ni kutumia siasa kuganga njaa zao,” alisema.
Alisema wananchi wanapaswa kuwa macho na wanasiasa
hao ambao malengo yao ni kuwaangamiza wananchi.

Akitaja baadhi ya sifa za wanasiasa aliowaita makanjanja, Nape alisema wengi wao ndiyo wanaotaka madaraka kwa gharama yoyote.
“Moja ya sifa kubwa ya wanasiasa hawa ni pamoja na kutaka madaraka kwa gharama zozote hata ikiwa ni pamoja na kuondoa uhai wa mtu,” alisema.
Alisema Chadema wanachojua kwa sasa ni kuwahujumu wale wote wenye mawazo tofauti na yao kwa kuwatesa na hata kupoteza maisha ya wanaowapinga.
“Badala ya kushindana kwa hoja na sera, wanachokijua wao ni kung’oa kucha za wanaowapinga, kuwatesa na wakati mwingine hata kumwaga damu kwenye operesheni zao,” alisema.

Alisema kwa kuwa wamekusudia kwa gharama yoyote kushika dola, hawajali damu za Watanzania zinazomwagika ili mradi wanafanikisha wanalolitaka.Akikumbushia operesheni mbalimbali zilizofanywa na Chadema nchini tangu uchaguzi uishe mwaka 2010, Nape alitoa mifano ya operesheni ya mjini Arusha, Morogoro, Iringa, Singida na kwingine ambako maisha ya baadhi ya Watanzania yalipotea lakini hawakushtuka wala kuwajibika.

“Tunamwamini Mungu hataruhusu damu hizi ziendelee kumwagika kisa wanasiasa makanjanja, pia laana ya damu hizi zilizomwagika zitaviua vyama hivi na nchi yetu itabaki salama,” alisema.
Nape alitoa wito kwa wananchi kuwa macho dhidi ya wanasiasa wa namna hiyo.
“Hewa wanayovuta wanasiasa makanjanja ni ya watu wanaowaunga mkono, tunaweza kuamua leo kuwanyima hewa hiyo na huo ndiyo utakuwa mwisho wao,”alisema Nape.

SOURCE::MWANANCH

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top