Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WABUNGE WASHAURIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA KUANZISHA BENKI ZA JAMII


WABUNGE
Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma.
SERIKALI inahakikisha kuwa inaweka mazingira bora na salama ya kiuchumi ili kuwezesha sekta binafsi kuanzisha mabenki na kutoa huduma bora za kibenki kwa wananchi.
Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo Mbunge wa Kwela Mhe. Ignas Aloyce Malocha aliuliza swali kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha akitaka kujua ni lini Serikali itashawishi taasisi za kifedha kuanzisha matawi yao katika mji mdogo wa Laela.
Naibu Waziri Fedha Mhe. Saada Mkuya Salumu kwa niaba ya Waziri Fedha alisema kuwa serikali inatambua umuhimu wa wananchi kupata huduma za kibenki karibu na maeneo yao na pia serikali inatambua kuwa huduma hizo za kibenki kwa wananchi kazima ziwe zenye faida kwa pande zote mbili yaani kwa mabenki na wateja.
Naibu Waziri aliongeza kuwa kwa kuzingatia sera ya sasa ya huduma za mabenki, waheshimiwa Wabunge wanaweza kushirikiana na Serikali katika kuwahamasisha wananchi kujiunga na kuanzisha benki za jamii (Community banks) zinazozingatia mazingira ya mahali husika pamoja na kuzihamasisha benki zilizopo nchini kufungua matawi katika maeneo hayo.
“Serikali kwa kutambua umuhimu wa suala hili, imewasiliana na Benki ya NMB ambao wamekubali kwenda Laela kutathmini mazingira ya kibiashara kabla ya kufungua tawi mahali hapo”. Alisema Naibu Waziri huyo.
Akijibu maswali mawili ya nyongeza toka kwa mbunge huyo ambayo yalitaka kujua kwanini serikali isitumie Mobile Banking na kwanini benki hutoza riba kubwa, Mhe. Mkuya alijibu kwa kusema kuwa serikali haitumii mobile banking hivyo itashawishi benki nyingine zianzishe huduma hizo.
Kuhusiana na riba kubwa itozwayo na mabenki, Naibu Waziri alisema kuwa riba kubwa inategemea na benki zenyewe zinavyotumia gharama kubwa na riba katika kutoa huduma hivyo nao hawanabudi kupandisha riba kwa wateja wao.
Serikali kupitia Benki Kuu, imeweka sheria na taratibu za kusaidia juhudi za wananchi katika kuanzisha mabenki au taasisi za fedha katika maeneo yao. Serikali pia inayo sera ya Taifa inayolenga kuhamasisha uanzishwaji wa mabenki kwa ajili ya wateja wadogo (National Microfinance Policy) na sera hii inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top