Wabunge
wameendelea kushambuliana kwa maneno makali huku Mbunge wa Viti Maalumu, Ester
Bulaya (CCM) akimtuhumu mbunge mwenzake wa Viti Maalumu bila ya kumtaja jina
kuwa anatumia fedha zake kuyumbisha sheria.
Mbunge
huyo alisema kuwa kigogo huyo amekuwa akitumia fedha nyingi kupindisha sheria
ili nyumba yake iliyoko eneo la Kawe Dar es Salaam isivunjwe licha ya kuwa iko
katikaeneo la wazi.
Alitoa
shutuma hizo wakati akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa
Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano kwa mwaka wa Fedha 2013/14.
“Nimejifunza mambo mengi jeshini, miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kusema
ukweli kwa ajili ya nchi yangu na watu wake, na nitasema kweli daima fitina
kwangu ni mwiko,” alisema Bulaya na kuongeza:
“Yupo
mtu hapa ambaye ni kigogo mkubwa na kiongozi mkubwa wa kisiasa ambaye yupo humu
ndani, lakini amekuwa akitumia fedha zake kuiyumbisha sheria na kuzuia nyumba
yake isivunjwe, hili ni jambo la hatari sana mheshimiwa spika naomba kutoa hoja
kuwa nyumba hiyo ivunjwe ndani ya siku saba,”
Eneo
hilo limekuwa na migogoro ya muda na baadhi ya nyumba zilivunjwa na Serikali
lakini nyumba hiyo inayotuhumiwa kuwa ya mbunge aliyekwenda mahakamani kuzuia
nyumba yake isivunjwe.
Bulaya
aliitaka Ofisi ya Makamu wa Rais kutoogopa kuvunja nyumba hiyo kwani bila ya
kufanya hivyo jamii haitawaelewa.
“Kutokana
na hilo, niko tayari kutoa shilingi ili kuzuia bajeti hiyo kama sitapata majibu
ya kuridhisha juu ya nyumba hiyo, kwani hatutendi haki kama viongozi ambao
tunatakiwa kuwa ni mfano kwa wengine juu ya mema lakini tunaongoza kufanya
maovu,” alisisitiza Bulaya.
Hata
hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alitoa ufafanuzi na kumtaka Bulaya kuwa
mvumilivu kwani mahakama ndiyo chombo pekee kitakachotoa uamuzi wa mwisho juu ya
haki ina nani na inafaa kutolewa
lini.
SOURCE::MWANANCHI::

Post a Comment