Washindi wa kipindi cha Nne cha Guinness Football Challenge, Enphatus
Nyambura(kushoto) na Samuel Papana(kulia) katika picha ya pamoja na
watangazaji wa kipindi hicho Larry Asego and Flavia Tumsiime jana baada
ya ushindi.
Aprili 10, 2013, Dar es Salaam; Katika sehemu ya nne jana usiku kupitia
televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalikuwa na ushindani mkubwa lakini washiriki kutoka Kenya Enphatus
Nyambura na Samuel Papa waliweza kumudu vishindo na kufanikiwa kuwa timu ya
tatu kutoka Kenya kuingia katika hatua ya Pan- Africa. Katika kipindi hiki cha
nne washiriki walijitahidi kufanya vizuri katika kuonesha uwezo wao wa kuchezea
mpira na kujipatia alama nyingi japo walishindwa kujibu maswali kwa
ufasaha.Washiriki kutoka Kenya walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya
kulenga ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia fedha
za kimarekani dola 1,500.
Enphatus na Samwel wana
nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo
wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita
cha fedha za kimarekani hadi kufikia
dola 250,000. Katika sehemu ya tano ya mashindano
haya, yanayorushwa na vituo vya Televisheni vya ITV na Clouds TV timu nne mpya zitaingia
uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi na kuendelea na mashindano hata kuingia hatua
ya Pan-African. Je timu nyingine ya Kenya inaweza kushinda?
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya
Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila
Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia
saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku
ambapo Clouds TV itarusha kipindi
hicho saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .
Tafadhali kunywa
kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18
Post a Comment