Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANA LAMBALAMBA AZAM FC SASA KUPEPETANA NA FAR RABAT YA MORROCO!!


1 (2)
Wachezaji wa timu ya Azam FC Brian Umony jezi namba 9 na John Bocco jezi namba 19 wakiruka juu katika lango la timu ya Barrack katika mchezo wa kombe la Shirikisho ambapo timu ya Azam imefuzu na kutinga raundi ya tatu ya michuano hiyo baada ya kutoka suluhu ya 0-0 kwenye uwanja wa Taifa IMG_2410
 
Mchezaji Kipre Chetche wa Azam akikwatulia karibu na eneo la hatari na wachezaji wa timu ya Barrack kwenye mchezo wakombe la Shirikisho uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo.
…………………………………………………………………………
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es Salaam
Mabingwa mara mbili wa kombe la mapinduzi na makamu bingwa wa kombe la Kagame, klabu ya Azam Fc yenye makazi yake Mbande ChamaziComplex imefanikiwa kufuzu raundi ya tatu ya kombe la shirikisho licha ya leo hii kutoka suluhu pacha ya bila kufungana dhidi ya klabu ya Barrack Yc kutoka nchini Liberia.
Akizungumza na matandao huu muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga amesema wamepokea vizuri matokeo ya mchezo huo ingawa hesabu zao zilikuwa kupata ushindi wa nyumbani.

“Mpira wakati Fulani hukataa, leo bahati haikuwa yetu kabisa, tumejaribu kutengeneza nafasi lakini hatukufanikiwa kufunga, wengi watajiuliza sana, kila mtu akumbuke kuwa wachezaji walioshindwa kufunga leo,ndio wale waliofunga mabao mawili kule Monrovia nchini Liberia”. Alisema Idd.
Idd alisema ushindi wa ugenini wa 2-1 umewafanya wasonge mbele ingawa Barrack Yc walikuwa wanahitaji ushindi kama walivyofanya kwao, lakini wamekumbana na kisiki cha mpingo leo uwanja wa taifa.
“Baada ya mchezo huo, kocha wetu mwiingereza Sterwart Jan Hall ameridhika na matokeo, kilichobaki na kuangalia hesabu za ligi kuu soka Tanzania bara kabla ya kuanza kuwaangalia wapinzani wetu siku zijazo”. Alisisitiza Idd.
Pia alisema kuwa watanzania wengi walidhani timu ya Barrack YC ni nyepesi baasa ya kuwafungwa kwao, lakini kiukweli ni timu ambayo imejipanga vizuri na ndio maana leo imewatoa jasho uwanja wa taifa baada ya kutoka nao 0-0.
“Unajua leo kila timu ilakaza kupata matokeo ya ushindi, tulishambuliana kwa zamu, lakini kwa upande wetu washambuliaji wetu kama John Bocco, Kipre Herman Tchetche walikosa nafasi za kufunga, yote kwa yote ni mchezo wa soka bwana”. Alisema Idd.
Afisa habari huyo aliongeza kuwa bbaada ya matokeo ya leo, sasa wanajipanga kukutana na timu ya jeshi la Morroco, kutokea kaskazini mwa bara la Afrika, FAR Rabat ambao ni wagumu kushindwa.
Katika mchezo huo wa kukata na shoka, kikosi cha wana lambalamba Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, Joackins Atudo, David Mwantika, Kipre Balou, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’, Humphrey Mieno/Abdi Kassim na Brian Umony/Khamis Mcha ‘Vialli’.
Barack Y.C ya Liberia mashine zao zilizoanza zilikuwa.; Winston Sayouah, Karleo Anderson, Joseph Broh/Prince Kennedy, Cammue Tummomie, Prince Jetoh, Junior Barshall, Benjamin Gbamy, Abraham Andrews, Randy Dukuly/Erastus Wee, Mark Paye na Ezekiel Doe.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top