Katibu Mkuu wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (kulia) akiangalia picha
ya nembo ya chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria aliyopewa na
Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John
(kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya
wanajeshi 22 kutoka chuo hicho wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku
tano
Katibu Mkuu wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (kulia) akimkabidhi picha
ya kinyago cha ujamaa Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja
Generali Ati John (kushoto) wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na
Unadhimu walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao
kutoka nchini Nigeria wako ziara ya mafunzo ya siku tano
nchini.
Mkurugenzi wa kikosi cha
Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John (kushoto) akimwelezea Katibu
Mkuu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda
kuhusu picha ya kinyago kinachoonyesha mtawala wa makabila mbalimbali ya nchi
hiyo alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanajeshi
22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wako nchini kwa
ziara ya mafunzo ya siku tano.
Katibu Mkuu wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (kulia) akimkabidhi picha
ya wamasai Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali
Ati John (kushoto) wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu
walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Kanali Anderson Msuya
(kushoto) kutoka Jeshi la Wananchi la wa Tanzania (JWTZ) akiongea jambo na
Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John
wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipoitembelea wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Mchezo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanajeshi 22
kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakimsikiliza Katibu
Mkuu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda
(hayupo pichani) wakati walipomtembea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya
Filamu na Michezo ya kuigiza Joyce Fisoo akielezea kuhusu kazi za bodi hiyo kwa
wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria
walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Joyce Hagu ambaye ni Kaimu Mkurugenzi msaidizi Idara ya
utamaduni.
Wanajeshi
22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakiwa katika picha
ya pamoja na wafanyakazi wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
wakati walipoitembelea wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao
kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku
tano.Picha na Anna Nkinda-MAELEZO
Post a Comment