Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WATOTO ELFU KUMI NA SITA WAPEWA TIBA YA MALARIA BURE

 
 
1ZAIDI watoto elfu kumi na sita wenye umri wa miezi mitatu hadi miaka
mitano kutoka katika Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga wamefanikiwa
kupatiwa matibabu bure ya Malaria na wahudumu wa afya za msingi.
Hayo yamebainishwa na Bw Julius Massaga (pichani)ambaye ni mkurugenzi wa
kuratibu na kukuza utafiti kutoka katika Taasisi ya Kitaifa ya utafiti
wa magonjwa ya Kibinadamu (NIMR)wakati akizungumza kwenye Kongamano la
27 la hiyo pamoja na kongamano la pili la Afya Moja Afrika
linaloendelea Mjini hapa.
Massaga alisema kuwa watoto hao wamefaidika kupatiwa matibabu bure
kupiotia mradi unaoendeshwa chini ya Taasisi ya NIMR ambapo umelenga
kupambana na kuepusha vifo vinavyotokana na Malaria ndani ya Wilaya
hiyo ya Pangani.
Alisema kuwa hapo awali mradi huo ulilenga kusaidia watoto ambao
wanatokea katika mazingira ambayo huduma za afya ziko mbali na makazi
yao hali ambayo wakati mwingine inasababisha hata vifo wakati
wakiwaishwa kupatiwa huduma za afya.
“huu mradi ni endelevu na ulianza rasmi mwaka 2008 na sasa tunaingia
kwenye kipindi cha pili cha mapambano dhidi ya Malaria na
tutahakikisha kuwa hawa wahudumu wanapatiwa mafunzo ikiwa ni jinsi ya
kutumia vipimo ambapo wataweza kutoa dawa baada ya vipimo kwani hapo
awali walikuwa hawatumii vipimo”aliongeza Massaga.

Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja na kuwa hapo awali waliweza
kutoa elimu pamoja na vifaa kwa wahudumu wa afya ya msingi wapatao 59
lakini mpaka sasa kuna mradi huo ambao upo chini ya NIMR umeweza
kuonesha mafanikio makubwa sana kwa kuwa watoa huduma hizo wanatoa
wakiwa majumbani tofauti na huduma za afya za kawaida.
Aliongeza kuwa mradi huo ambao mpaka sasa umeweza kupunguza kwa
kiwango kikubwa sana kasi ya vifo vya Malaria kwa watoto wa maeneo
hayo ambapo pia kwa awamu nyingine ya mradi huo ambao unaanza May 2013
hadi May 2014 utasaidia pia kutoa elimu dhidi ya Malaria kwa kaya
mbalimbali.
“sisi tunaungana na Serikali katika mpango wake wa taifa wa kudhibiti
Malaria wameweza mradi huuu katika mpango wao wa Taifa huku sisi
tukiwa na malengo ya kuhakikisha kuwa tunapeleka Nchi Nzima lakini kwa
sasa tunatafuta matokeo mbalimbali ya ugonjwa huu wa Malaria ambao
mara nyingi unasababisha vifo”aliongeza Massaga
Alimalizia kwa kusema kuwa wao kama Taasisi ya Utafiti wanaendelea
kufanya tafiti mbalimbali juu ya Ugonjwa huo huku lengo likiwa ni
kuhakikisha kuwa Ugonjwa wa Malaria unatokomea kabisa.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top