"Nimeandika barua Kwa Spika wa Bunge kutaka Waziri wa
Nishati na Madini kutoa maelezo Bungeni kuhusu uamuzi wake wa kuwapa leseni
kubwa ya kuchimba #Uranium huko wilayani Namtumbo. Mnamo tarehe 10 Agosti 2013
Waziri alitamka ndani ya Bunge "sisi tunajua zaidi ya anavyojua yeye, Leseni
haijatolewa na haitatolewa mpaka Kampuni ya
#MantraResources ilipe kodi".
Kodi ya ongezeko la
mtaji (capital gains tax) ya $189m kufuatia mauzo ya mradi wa #MkujuRiverProject
kutoka kampuni ya Mantra kwenda kampuni ya AMRZ ya Urusi iligomewa kulipwa. #TRA
wamepeleka shauri hilo mahakama ya kodi na mpaka sasa maamuzi hayajatolewa. Kwa
mujibu wa mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2012, kabla ya Waziri mwenye dhamana ya
madini kubariki mauzo ya kampuni, anapaswa kupata Kibali Cha kwamba kodi zote
stahili zimelipwa. Kibali Kwa kampuni ya mantra kilitolewa bila kujali hitaji la
kisheria na sasa kampuni hii imepewa leseni.
Maamuzi haya ya Waziri
wa Nishati na Madini yanalikosesha Taifa mapato ya zaidi ya tshs 300bn ambazo
zingeweza kumaliza tatizo la nyumba za walimu nchi nzima na kulipia madai yote
ya walimu. Fedha hizi zingeweza kujenga barabara ya lami kutoka Manyoni mpaka
Itigi. Fedha zingeweza kukarabati reli ya Kati na kuirejesha katika ubora wa
unaotakiwa. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge nimetaka Waziri atoe maelezo bungeni
na wabunge wajadili. Ni dhahiri kwamba serikali inayoongozwa na CCM imeamua
kumaliza utajiri wote wa nchi na kuugawa Kwa wageni Kwa bei ya Che. Wananchi Ni
lazima kusimama imara kukataa uporaji huu na maamuzi haya ya kiburi Cha kudharau
Bunge yaliyoyafanywa na
Serikali."
Post a Comment