
Baada ya shutuma za rushwa ya ngono kuzidi kwa
waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, uongozi unaosimamia shindano hilo
umesema kama kuna mrembo yeyote ambae amewahi kuombwa rushwa hiyo ya ngono
ajitokeze.
Mkurugenzi Hashim Lundenga amesema “kuna kushutumiwa kwamba tunachukua rushwa ya ngono kutoka
kwa Wasichana kitu ambacho sio kweli, hakuna msichana aliesema ameingia kambini
au ameshinda kwa sababu ametoa rushwa ya ngono, katiba yetu inakataza kabisa
yeyote kujihusisha na hilo”

.
Moja ya kesi hizo ni pamoja na ya Mchungaji aliemuondoa
mwanae baada ya kupewa ubalozi wa kinywaji chenye kilevi, mrembo mwingine alikua
Nadya aliekua masomoni Chuo kikuu familia yake ilikataa kabisa mtoto wao
kushiriki.

.
Kwa kumalizia, Lundenga amekiri kwamba wanao utaratibu,
sheria na kanuni kwenye katiba yao ambayo imepitishwa na Serikali ikiwa na
maagizo mablimbali ikiwemo marufuku ya kiongozi yeyote kuomba rushwa ya
ngono.
Pamoja na kuzushiwa hizo kashfa, amesema idadi ya
Warembo wanaotaka kushiriki haijapungua bali imeongezeka kwa sababu Wasichana
ndio wanazidi kujitokeza.
Post a Comment