Lwakatare akimkumbatia kwa furaha wakili wake, Peter Kibatara, baada ya kufutiwa mashitaka ya ugaidi.
Askari wakimuamuru Lwakatare kuondoka kizimbani kwa ajili ya safari ya gerezani.
Ndugu, jamaa na wafuasi wa Chadema wakikumbatiana kwa furaha.
Mmoja wa wanachama wa Chadema akiwapigia simu wenzake kuwapasha kilichojiri mahakamani.
Ulinzi nje ya jengo la mahakama.
Wafuasi wa Chadema wakitoka mahakamani kwa furaha.
Kibatara akifafanua jambo kutoka kwenye makabrasha yake
Lwakatare akirudishwa rumande kwa kosa moja la kutaka kumwekea sumu, Dennis Msaki.
MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imemfutia mashitaka mawili ya ugaidi,
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Bw. Wilfred Lwakatare.
Jaji
aliyekuwa akiendesha shauri hilo, Lawrence Kiduri, amemfutia Lwakatare
mashitaka hayo na kumbakizia kosa la kujaribu kumwekea sumu, Mhariri wa
gazeti la Mwananchi, Dennis Msaki, ambalo dhamana yake iko wazi.
Akizungumza na gpl, wakili wa
mshitakiwa huyo, Peter Kibatara, amesema wanatarajia kumtoa kwa dhamana
mteja wake huyo siku ya Jumatatu ambayo anaamini kuwa taratibu zote
zitakuwa zimekamilishwa.
Post a Comment