|
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lucresia Makirie akimkabidhi pikipiki tatu |
Mwenyekiti
wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya
kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius
Kaijage
|
Mwenyekiti
wa kikosi cha Mafanikio Julius Kaijage akimkabidhi pikipiki mbili na
matairi 4 ya gari pamoja na mabati mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro
vifaa hivyo vyote vimetoka kwa wadau wa ulinzi mkoani hapa |
|
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiongea na wadau mbali mbali kwenye hafla
fupi ya kupokea misaada toka kwa wadau wa ulinzi mkoani hapa |
|
Mwenyekiti
wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya
kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius
Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi wanafanya kazi katika
mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha
analiwezesha kwa hali na mali. |
|
Meneja
wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lucresia Makirie
amesema benki yake imetoa msaada Pikipiki tatu kusaidia jeshi hilo ili
zisaidie katika ulinzi shirikishi katika mkoa wa Mbeya
|
|
Kamanada
wa Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athumani amewapongeza wadau mbalimbali
waliojitokeza kulisaidia jeshi hilo ambapo amewahahakikishia wananchi wa
mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya upo katika mazingira salama
kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi hilo . |
|
Picha ya pamoja
BAADHI
ya Wananchi Mkoani Mbeya wamelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa
kuendelea kusambaratisha na kumaliza kabisa mtandao wa ujambazi kutokana
na majambazi wengi kukamatwa na wengine kuawa.
Pongezi
hizo zimekuja Siku moja baada ya Jeshi hilo kuwauwa watu watano
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika majibizano ya kurushiana risasi
kati ya Askari na majambazi hayo katika tukio lililotokea katika kijiji
cha Garijembe Wilaya ya Mbeya.
Katika
kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea kufanya kazi katika mazingira
mazuri na kwa mafanikio na kuunga mkono juhudi zao, Wadau mbali mbali
leo wamejitokeza kulichangia jeshi hilo katika Hafla iliyofanyika
katika viwanja vya ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoani hapa.
Hafla
hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas
Kandoro Jumla ya Shilingi Milioni 28 zilipatikana vikiwemo vifaa mbali
mbali.
Mwenyekiti
wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya
kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius
Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi wanafanya kazi katika
mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha
analiwezesha kwa hali na mali.
Katika
Hafla hiyo Jumla ya Pikipiki tano zilinunuliwa ambapo kati ya hizo Tatu
zimetolewa na Benki ya Nmb kwa thamani ya Shilingi Milion 5.4, wakati
kamati ikinunua pikipiki Mbili kwa Thamani ya Shilingi Milioni Moja na
Laki Nane.
Mbali
na michango hiyo pia Wakala wa Majengo mkoa wa Mbeya (TBA) imetoa
mabati 22 ya Geji 28 yenye thamani ya Shilingi 460,000/=, pia kamati ya
Mafanikio imenunua Matairi nane yenye thamani ya Shilingi Milioni
3,020,000/=,pamoja na mafuta kwa ajili ya magari ambayo ni Lita 360 kwa
Mwaka zilizoahidiwa na kampuni ya G4S.
Mbali
na pongezi hizo Wananchi hao wamemshauri Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mbeya Diwani Athumani mbali na kupambana na uhalifu katika Mkoa wa Mbeya
na kuwasisitiza watu wanaofanya shughuli zisizokuwa na uhalali kuacha
mara moja au kuhama Mkoa pia wapendekeza kufanya ziara za kushtukiza
katika Vituo vidogo vya Polisi.
Kwa
upande wake Kamanada wa Polisi Mkoani hapa Diwani Athumani amewapongeza
wadau mbalimbali waliojitokeza kulisaidia jeshi hilo ambapo
amewahahakikishia wananchi wa mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya upo
katika mazingira salama kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi
na jeshi hilo .
Na Mbeya yetu
|
on Wednesday, May 8, 2013
Post a Comment