Kikosi
cha Zima moto na uokoaji cha Halmashauri ya mji wa Njombe kwa
kushirikiana na wananchi wakitoa mwili wa Mhandisi wa Maji katika
Halmashauri ya Mji wa Njombe Abdalah Mgambo baada ya kutumbukia kwenye
kisima hicho jana katika Uwanja wa ukumbi wa Turbo Mjini Njombe.
Mwili
wa Eng.Abdalah Mgambo ukionekana kwa umbali kwenye gari la Polisi
ukipelekwa hospitali Kibena kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
Wa
pili kushoto ni Mhandisi wa Maji Halamshauri ya Mji wa Njombe
Eng.Abdalah Mgambo enzi za uhai wake wakati wa Kilele cha Wiki ya Maji
March 22 mwaka huu katika kijiji cha Igominyi.
Marehemu
Abdalah Mgambo enzi za Uhai wake akisoma taarifa ya Hali ya maji katika
halmashauri ya Mji wa Njombe mwezi machi 22 mwaka huu wakati wa kilele
cha wiki ya Maji Igominyi Njombe.
Taarifa
toka eneo la Tukio zinasema kuwa marehemu Abdalah Mgambo alikuwa katika
Baa yake eneo la Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe kisha akamuaga mke wake
kwamba anatoka nje kujipumzisha kwenye gari lake majira ya Saa Moja
jioni jana April 30 akatoweka ghafla na kisha Kadi yake ya Benki ya NMB
Ilikutwa nje ya Kisima cha Maji kilichopo katika uwanja wa Ukumbi wa
Turbo Mjini Njombe.
Akizungumza na Mtandao wa www.gabrielkilamlya.blogspot. com eneo
la Tukio mara baada ya kuuokoa mwili wa Mhandisi huyo Afisa mtendaji wa
Kata ya Njombe Mjini Bwana Donald Mng'ong'o amesema kuwa leo asubuhi
amepata taarifa toka kwa mke wa marehemu kuwa alitoweka ghafla na mara
baada ya kuikuta kadi ya ATM nje ya kisima cha maji ndipo wakachukua
jitihada za kuanza kutafuta kwenye kisima hicho kwa kushirikiana na
kikosi cha Zima moto na Uokoaji cha Halmashauri ya Mji wa Njombe.
Bwana
Mng'ong'o amesema kuwa majira ya Tisa jioni mei mosi ndipo mwili wa
marehemu umeokolewa na kuwahishwa katika Hospitali ya Kibena Njombe.
Post a Comment