Timu ya CBE wakishangilia baada ya kupokea 500,000 taslimu baada ya kuivua ubingwa IFM |
Meneja wa bia ya Safari, Oscar Shelukindo akimkabidhi fedha taslimu 150,000 mchezaji Patrick Peter wa IFM baada ya kushinda kwenye mchezo wa mchezaji mmoja moja |
CBE wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa Mkoa wa Dar es Salaam |
CHUO Kikuu cha Biashara (CBE) jana kimetawazwa kuwa mabingwa
wa mchezo wa Pool Table mkoa wa Dar es Salaam baada ya kukivua ubingwa Chuo
Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwenye
mashindano ya Pool Table kwa Vyuo Vikuu vya Dar es salaam.
CBE ambayo imeingia fainali mara tatu mfululizo na kutolewa na IFM walionekana kupania mchezo
huo baada ya kuwaondoa mabingwa hao watetezi kwa mabao 13 kwa 4 kwenye fainali
zilizofanyika kwenye baa ya Meeda iliyopo Sinza, Kinondoni.
Baada ya CBE kuifunga IFM, walizawadiwa shilingi laki
500,000 na watawakilisha mkoa wa Dar es Salaam kwenye fainali za Pool Table
zitakazofanyika baadae hapa jijini Dar es Salaam na mshindi wa pili alizawadiwa
300,000.
Akizungumza na baada ya mchezo kumalizika , nahodha wa IFM Patrick Peter
alisema kweli wamesitikitishwa na kitendo cha kuvuliwa ubingwa ila
kwenye ushindani lazima mmoja apatikane tunakubali matokeo.
“Kwenye mchezo wowote mshindi ni mmoja na sisi tunakubali tumevuliwa
ubingwa kwa sababu wenzetu wametuzidi tunawatakia kila la heri”, alisema
Peter
Kwa mshindi mmoja moja Patrick Peter wa IFM alimfunga Salehe Amin wa
Chuo cha IAMCO na kuondoka na zawadi ya shilingi 150,000 pia
atawakilisha Dar es Salaam kwenye fainali za Taifa za mchezaji mmoja
mmoja.
Pia kulikuwepo burudani ya Joh Makini aka mwamba wa Kaskazini ambaye alitoa burudani ya kufa mtu na kuwapagawisha wanavyuo
Patrick Peter wa IFM akicheza pool table |
John Makini akitoa burudani |
Post a Comment