 |
| Mkurugenzi
wa Mafunzo na Organaizesheni wa Chadema Taifa Singo Bensoni alisema
Lengo la Mafunzo hayo ni kuhakikisha wanapata wakufunzi 30606 nchi nzima
ambao watatawanyika katika kila kitongoji nchi nzima kwa ajili ya kutoa
elimu kwa wananchi na kuunda matawi ya Chama hicho ikiwa ni pamoja na
kukifikishama hadi ngazi ya Chini |





 |
Hoteli ya Golden City ya Jijini Mbeya.
Chama
Cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA) kimeendesha mafunzo kwa wanachama
wake 81 ambao wanatoka katika Majimbo 27 ya Uchaguzi katika Kanda ya
Nyanda za Juu kusini Mafunzo yanayofanyika Katika Ukumbi wa Hoteli ya
Golden City ya Jijini Mbeya.
Mkurugenzi
wa Mafunzo na Organaizesheni wa Chadema Taifa Singo Bensoni alisema
Lengo la Mafunzo hayo ni kuhakikisha wanapata wakufunzi 30606 nchi nzima
ambao watatawanyika katika kila kitongoji nchi nzima kwa ajili ya kutoa
elimu kwa wananchi na kuunda matawi ya Chama hicho ikiwa ni pamoja na
kukifikishama hadi ngazi ya Chini.
Alisema
mafunzo hayo yalianza kutolewa kwa kuchukua wakilishi watatu kila Jimbo
la Uchaguzi ambao baada ya kumaliza watafanya mitihani na kufuzu kuwa
wakufunzi wa chama na kuongeza kuwa mbinu itakayotumika ni kuendesha
mafunzo ya chini kwa chini bila kuvaa sare za chama wa kutumia magari ya
matangazo na vipaza sauti.
Aliongeza kuwa katika mafunzo hayo yanahusisha wawakilishi wawili kila
kanda ambao waliungana na wanachama wengine 10 wa Kitaifa ambao jumla
walikuwa 30 ambao baada ya kufuzu mafunzo walirudi kufundisha katika
kanda zao ambapo katika Kanda ya Mbeya ina wanafunzi 81,Arusha 96,
Mwanza 72 na Shinyanga 60 ambao wanawakilishwa na watu watatu kila Jimbo
la Uchaguzi.
Aidha alisema mafunzo hayo yanatolewa kutokana na ufadhili wa watu wa
Ujerumani na kwamba wakufunzi hao watapewa Miezi miwili kuhakikisha
wameyafikia maeneo yote nchini na kufanikiwa kuwapa elimu wananchi
wapatao 30 kwa Mtu mmoja na kuunda Msingi tayari kwa maandalizi ya
Uchaguzi mkuu ujao.
Na Mbeya yetu
|
on Saturday, May 11, 2013
Post a Comment