MAJASUSI wa shirikisho la ujasusi la
nchini Marekani wamefika jijini Arusha kusaidiana na wapelelezi wa nchini
Tanzania katika uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa bomu kwa
waumini wa kanisa katoliki na Balozi wa Vatican nchini siku ya
jumapili.
Magesa alitoa taarifa hiyo wakati akitoa taarifa ya
Mkoa kwa waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipozuru
eneo la tukio na kuwatembelea wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali na
kuwapa pole.
Wakati maafisa hao wakifika jijini humo tayari vyombo
vya usalama vinawashikilia watu zaidi ya 10 miongoni mwao wakiwemo watu wanne
kutoka Saudia Arabia ambao waliwasili nchini kupitia uwanja wa
ndege wa Kilimanjaro(KIA) siku moja kabla ya tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa watu
hao walikamatwa muda mfupi wakiondoka nchini kupitia mpaka wa
Namanga kuelekea nchini Kenya baada ya tukio kutokea.
Hata hivyo taarifa hiyo haikuweza kutoa ufafanuzi zaidi
na kwamba taarifa zaidi juu ya upepelezi zitatolewa kadri muda na wakati
utakavyoruhusu.
Post a Comment