NWashindi wa kwanza wa nusu fainali ya kwanza ya Guiness Football Challengekutoka Ghana Naab Jonathan Baan(kushoto) na Desmond Odaano(kulia) katika picha ya pamoja na waendeshaji wa kipindi cha Pan-Africa Guinness Football Challenge Larry Asego na Mimi Kalinda.
************
Mei 23 2013, Dar es Salaam: Jana usiku kupitia
televisheni za ITV na Clouds TV nusu fainali ya kwanza kabisa ya GUINNESS®
FOOTBALL CHALLENGE™ ilirushwa hewani na katika runinga Afrika nzima ambapo timu ya Ghana ilionesha ni kwanini ni timu bora ambayo ndiyo imejishindia pesa
nyingi mpaka sasa.
Jonathan
Nabb na Desmond Odaano walionesha uwezo na ujasiri wao walipoibuka washindi zidi ya
wapinzani wao timu kutoka Kenya katika mchezo wa jana.
Katika hatua ya pesa
ukutani walifanikiwa kulenga lango namba nne na hivyo kupata dola za kimarekani
12,000 wanazoziongeza katika dola 8,500 walizokuwa nazo awali katika hatua ya
robo fainali.
Wakenya
Francis Ngigi na Kepha Kimani ambao ni washindi wa pili katika nusu fainali hii
wataungana na Ghana katika fainali. Ingawa waliikosakosa hatua ya ukuta wa pesa
wa Guinness bado wana nafasi ya kuwa
mabingwa katika fainali.
Post a Comment