Takwimu hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, ambaye alisema kuwa viwango hivyo
vimetokana na utafiti uliofanywa kati ya Februari hadi Oktoba mwaka jana
2012.
Kwa mujibu wa naibu waziri, utafiti huo ulifanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Alikuwa akijibu swali la Abdallah Haji Ali
(Kiwani–CUF) aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu utumiaji wa pombe
ambao umethibitika kuwa ni hatari kwa afya za binadamu.
Naibu waziri alisema tafiti zimeonyesha kuwa watu
milioni mbili wanafariki dunia kila mwaka duniani kutokana na madhara ya
matumizi ya pombe na asilimia nne ya matatizo ya kiafya yanatokana na
matumizi ya pombe.
“Hali inazidi kuwa mbaya zaidi katika nchi
zinazoendelea hasa kutokana na kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi na
ustawi wa jamii inayochangiwa na magonjwa ya malaria, kifua kikuu na
Ukimwi,” alisema Dk Rashid.
Naibu Waziri alisema kutokana na kuongezeka kwa
athari zitokanazo na matumizi ya pombe hasa kwa magonjwa yasiyo ya
kuambukiza, Serikali inatekeleza mkakati wa kukabiliana na magonjwa ya
kuambukizwa unaoelekeza kutoa elimu kwa wananchi kupitia njia
mbalimbali.
Kuhusu mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo,
alisema tayari Serikali imeanza utaratibu wa kuziwezesha hospitali za
rufaa za mikoa, kuanza kutoa huduma kwa waathirika wa matumizi ya dawa
za kulevya na pombe.
Post a Comment