Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Rombo, Judethadeus Mboya |
Mkuu wa Sekondari ya Tanya, Victus Kiwango |
Mkuu Msaidizi wa Sekondari ya Nduweni, Venance Mramba |
Na Thehabari.com, Rombo
CHAMA
cha Walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Rombo kimesema shule nyingi za
Sekondari za Kata wilaya hiyo na maeneo mengine nchini zinajiendesha kwa
kutegemea fedha za mifukoni kwa walimu wakuu wanaoziongoza shule hizo.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Katibu wa CWT Wilaya ya Rombo, Erasmo Mwingira
alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi. Hata hivyo
uchunguzi uliofanywa na gazeti hili hivi karibuni kwa kutembelea shule
kadhaa za sekondari wilayani hapa umebaini kuwepo na mazingira magumu ya
uendeshaji wa shule hizo kutokana na ugao wa fedha za uendeshaji shule
hizo kutokuwa wa uhakika huku hata kiasi kinachozifikia hakitoshelezi
gharama za uendeshaji.
Post a Comment