Gari la wagonjwa la Manispaa ya Masasi likiteketea kwa moto baada ya kutokea vurugu leo.
Barabara ikiwa imefungwa kwa kuweke magogo na mawe.
Mkazi wa Mtwara akinawa uso baada ya kupigwa mabomu ya machozi.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa katika doria.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa katika doria ya miguu.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa katika doria..
Magari ya Watumishi wa Umma yakiungua kwa moto.
Ofisi za Elimu Masasi.
Mitaa kadhaa ikiwa haipitiki baada ya kuchomwa matairi ya gari.
Mtwara, Tanzania
Mtwara, Tanzania
Mtu
mmoja amefariki dunia na wengine 21 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi
kutokana na vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara leo, zilizosababishwa na
makundi ya vijana kuchoma moto, majengo ya ofisi za umma, nyumba za watu
na kufunga barabara.
Hali
hiyo imetokana na hotuba ya Waziri wa Nishati Prof. Sospeter Muhongo
akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi
linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar wakati kauli mbiu ya Wananchi wa
Mtwara ni "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni"
Wananchi
walalamikia kituo cha Television na Radio TBC kuzuia na kukata mawimbi
yake kutoonekana wala kusikika katika Mkoa wa Mtwara kwa muda.
Kufuatia
Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la
gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam wakati Waziri wa Nishati akisoma
hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi
linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam Wananchi wa Mtwara
wakacharuka!
Kufuatia tukio hilo Daraja la Mikindani limevunjwa na wananchi wenye hasira pamoja na kuchoma moto Jengo la Ofisi ya CCM saba saba.
Nyumba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia yachomwa moto.
Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa
Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwa ajili ya operation
inayoendelea imechomwa moto.
Kutokana na
hali hiyo watu walikimbia ovyo mitaani na watoto wamefungiwa mashuleni
huku walimu walimu pia wakikimbia kutoka katika vituo vyao vya kazi.
Katika maeneo ya Magomeni-Mtwara milio ya irsasi na mabomu ya machozi ndio ilikuwa imetawala na kusababisha hofu kubwa.
Kutokana
na hali hiyo huduma zote za kijamii zimefungwa hakuna usafiri, masoko,
maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi
kazi. Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la
polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato
wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.
Post a Comment