Watangazaji wa Nuru FM kutoka
kushoto Shadrack Mwansasu na Yusta Msowoya kulia wakimpa pore
mtangazaji mwenzao Husein Farahan ambae leo alikamatwa na polisi wakati
akielekea kazini na kuchezea kipigo na kuwekwa rumande
Mwili wa mtangazaji Husein Farahan ukiwa umevimba baada ya kichapo kutoka kwa askari wa FFU leo
Kichapo kilikuwa kikali kweli asimulia mtangazaji huyo
Mtangazaji wa kituo cha Nuru FM Husein
Farahan amesimulia kilichomkuta kuwa alikuwa katika usafiri na boda
boda na kusimamishwa na polisi kabla ya kuchezea kipigo
Mtangazaji huyo alisema kuwa alikamatwa
eneo la Mshindo baada ya askari hao kumsimamisha na kuanza kutembeza
kipigo na kuwa amepatwa na majeraha mgongoni kutokana na kupigwa
virungu mtindo mmoja.
Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa
Iringa Michael Kamuhanda amesema kuwa mbali ya mtangazaji huyo
kukamatwa pia wapo askari polisi waliokamatwa kutokana na
kutofahamika na kuwa askari hao ni wanachuo ambao wapo mjini hapa
kimasomo japo kwa sasa wameachiwa huru.
Kamuhanda amesema kuwa waliokamatwa
hadi saa 3 usiku walikuwa ni watu zaidi ya 100 na kuwa baadhi yao
wameachiwa na wanaoendelea kushirikiliwa ni 80 na kesho asubuhi
watafikishwa mahakamani .
|
Post a Comment