Na Gervas Mwatebela, Dar es salaam
Utafiti
wa kisayansi umebaini kuwa mbu jike wanaoambukiza vijimelea vya ugonjwa
wa Malaria huvutiwa zaidi na harufu ya mwili wa binadamu kuliko wadudu
wengine.
Watafiti
waliochapisha matokeo ya utafiti wao katika jarida la Plos One,
wanaamini kuwa Mbu wanaobeba viini vinavyosababisha Malaria, huwa na
uwezo mkubwa wa kunusa.
Daktari
James Logan, kutoka chuo cha mafunzo ya fya mjini London, anasema kuwa
moja ya mambo ambayo humshangaza ni ambavyo viini vinakuwa na akili
nyingi.
Anasema kuwa viini vinaonekana kuwa na akili nyingi kiasi cha kuwa mbele kwa fikira kuliko hata wanasayansi.
Katika kufanya utafiti wao, wanasayanyi waliwaambukiza Mmbu na viini hatari vya Plasmodium falciparum.
Waliwaweka
Mmbu hao katika mkebe pamoja na soksi ilyoikuwa inavunda na ambayo
ilikuwa imevaliwa kwa masaa ishirini. Mmbu hao walijazana kwenye soksi
hiyo,Wanasayansi hao walifanya utafiti huo na Mmbu ambao walikuwa hawana
viini hivyo.
Waligundua kuwa Mmbu waliokuwa na viini waliweza kuvutiwa zaidi na soski zilizokuwa na uvundo.
Wanasayansi
wanaamini kuwa Mmbu waliokuwa na viini wanakuwa na uwezo mkubwa zaidi
wa kunusa kwa sababu viini ndivyo vinawawezesha kunusa zaidi.
Kwa
Mbu, binadamu anakuwa rahisi kushambulia kwa sababu ya harufu ya mwili
wake na kisha viini hivyo ninavamia damu yake kuhakikisha kuwa
vinaendelea kuzaana.
Watafiti hao sasa watafanya utafiti wa miaka mitatu kutaka kujua ni vipi viini vina uwezo wa kufanya hivyo.
Daktari Logan , anasema kuwa ikiwa wataweza kujua viini vinavyosababisha Malaria, itawasaidia kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Kulingana
na takwimu za hivi karibuni, shirika la afya duniani linasema kuwa
mnamo mwaka 2012, takriban watu milioni 219 waliugua Malaria huku
wengine 660,000 wakiripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo.
Afrika
ndilo bara lenye visa vingi vya watu kuugua Malaria na asilimia tisini
ya vifo vinavyotokana na Malaria hutokea barani humo.
Post a Comment