Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa alipowasili Ijumaa usiku tayari
kujiunga na viongozi wenzie wa nchi za Afrika katika sherehe za miaka 50
tangu kuanzishwa kwa Umoja wa nchi za Afrika (AU)
zinazofanyika leo katika makao makuu ya umoja huo
Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiwasili Addis Ababa
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipata maelezo ya maandalizi
ya sherehe hizo toka kwa balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Profesa Joram
Biswaro mara baada ya kuwasili Addis Ababa
*********
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni miongomi mwa marais wa bara la
Afrika watakaohudhuria Sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa
Umoja wa nchi za Afrika (AU) zinazo fanyika rasmi leo Jumamosi Mei
25, 2013 katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Shamrashamra zimetawala kila pembe ya jiji la Addis, wakati
viongozi wa nchi za Afrika wakiwasili mmoja baada ya mwingine katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Bole.
Muungano wa Afrika wakati huo ukijulikana kama OAU,
ulizaliwa Mnamo Mei 25, 1963 jijini Addis Ababa, ukianza na nchi za 32 na
baadaye nchi 21 zikajiunga miaka ilivyozidi kwenda, huku Afrika ya kusini
ikijiunga kuwa mwanachama wa 53 mwaka 1994.
Mwaka 2001 OAU iligeuzwa kuwa AU katika mkutano uliofanyika
Lusaka, Zambia. Jumamosi hii kutakuwa na sherehe za kilele kuadhimisha miaka
hiyo 50 ya AU na kuhudhuriwa na marais karibia wote wa Afrika.
Kauli mbiu ya sherehe za hapo kesho ni mjadala mkuu kuhusu
ushirikiano wa nchi za Afrika na kuimarishwa kwa muungano huo. Mwenyekiti wa
tume ya muungano huo, Dr Nkosazana Dlamini Zuma, anaseme kuwa hii itakuwa fursa
kwa AU kujadili kuhusu uwezo wa bara hili na ambacho kinaweza kufikiwa katika
miaka 50 ijayo
Post a Comment