KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Abdulrahman Kinana amesisitiza kwamba Chama kitamwadhibu bila
huruma mwanachama yeyote anayejipitisha-pitisha katika maeneo mbalimbali
na kufanya kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.
Kinana alisema hayo leo wakati
akizungumza na Kamati ya Siasa na mkoa wa Iringa, katika kikao maalum,
kilichofanyika kabla ya kwenda mkoani Njombe ambako ameanza ziara ya
siku saba mkoani humo.
Kinana alisema, katazo la
wanachama kujipitisha-pitisha na kupiga kampeni za kuwania urais au
nafasi yoyote kabla ya muda halitoki midomoni mwa viongozi bali ni kwa
mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama.
“Ndugu zanguni, nawakumbusha
kwamba kwa hili hatuna mzaha nalo, hivyo hakikisheni kila mmoja wenu
kama kiongozi hajihusishi kwa namna yoyote kushiriki katika kutumiwa na
wanachama hao wanaojipitishajiptisha”, alisema Kinana na kuongeza;
“Ni lazima Chama kiwe kikali
kwenye jambo hili, kwa sababu kama kitawaacha watu hawa kukiuka taratibu
na kanunzi za Chama wanazidi kukifanya chama kuwa na makundi mengi
ambayo yatakipeleka pabaya,” alisema Kinana
Kinana alisema, kazi walioyonayo
wale wote wanaokitakia mema Chama, ni kumuunga mkono Mwenyekiti, Rais
Jakaya katika kazi ya kuhakikisha CCM inakamilisha utekelezaji ilani
yake ya Uchaguzi kwa kiwango kinachostahili na siyo muda kujipitisha
pitisha mtu binaafsi kwa wanachama huku utekelezaji wa ilani ukisinzia.
Alisema kuwa hivi sasa kazi ya CCM
ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya uchaguzi kwa kipindi kilichobaki
cha miaka miwili ya nusu kabla ya kumalizi kwa awamu ya uongozi wa Rais
Jakaya Kikwete.
“Ni wazi kazi yatu CCM ni
kuhakikisha tunatekeleza ilani ya uchaguzi kwa vitendo na si mamneno
kama wanavyofanya wengine. ni kazi kubwa imefanyika chini ya uongozi wa
Rais Kikwete na katika kipindi cha miaka miwili iliyobaki tumedhamiria
kuifanya zaidi”,
Alisema moja ya maeneo ambayo
licha ya kuwepo changamoto za hapa na pele lakini yamefanikisha sana
utekelezaji wa ilani ya CCM, ni kwenye Halmashauri mbalimbali nchini
ambapo watendaji walio wengi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutekeleza
miradi ya maendeleo kwa kasi.
“Kwa kweli CCM lazima hawa
tuwapongeze maana kuna wengine kazi yao imebaki kuwashambulia huku
wakijua watendaji hao hawana fursa ya kujitete mbele ya jamii. chapeni
kazi nasi tupo nyuma yenu, na kila wakati tutakuwa tukitambua juhudi na
kazi kubwa mnayoifanya kwa jamii,” alisema Kinana.
Akizungumzia uchaguzi mdogo wa
madini unaofanyika katika kata mbalimbali nchini Kinana, alisema CCM
itashinda uchaguzi huo kwenye kata zote 25 kutokana na mtandao wa chama
chake na imani inayoonekana kuwepo kwa wananchi juu ya CCM.
Post a Comment