Waziri Asiye na Wizara Maalum wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Machano Othman akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni
10 nahodha wa timu ya KMKM, Maulid Ibrahimu baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu
ya Grand Malt huko Zanzibar. (Na Mpiga Picha Wetu
Wachezaji
wa timu ya KMKM wakiwa
katika picha ya pamoja na kombe lao wakishangilia ubingwa wa soka wa Ligi Kuu ya
Soka ya Grandmalt huko Zanzibar.
Timu
ya KMKM wakiwa pamoja na kocha wao Ally Bushiri wakishangilia ubingwa wa Ligi
Kuu ya Soka ya Grand Malt huko Zanzibar.
Na
Mwandishi Wetu, Zanzibar
MABINGWA
wapya wa Ligi Kuu ya Grand Malt, KMKM imesema itahakikisha inafanya kweli katika
mashindano mbalimbali ili kudhihirisha umma kuwa, kinywaji hicho hakikukosea
kuidhamini ligi hiyo.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi washindi zawadfi iliyofanyika kwenye hoteli ya
Zanzibar Ocean View, Afisa Michezo wa KMKM, Ramadhan Hassan ‘Mabio’ alisema hilo
watalifanya pamoja na pia kuilinda heshima ya
timu.
“Timu yetu
ni moja kati ya zile kongwe hapa Tanzania, hivyo napenda kuahidi kwamba
tutafanya kila iwezalo ili kuwafanya wadhamini wetu wajisikie furaha kwa
kushinda kwa mechi tutakazocheza.
“Kwa muda
mrefu soka la Zanzibar lilikuwa limeyumba kutokana na kukosa mdhamini, ila kwa
sasa tunapenda kuwashukuru Grand Malt kwa kudhamini Ligi Kuu ya Zanziobar,”
alisema.
Maneno hayo
yaliungwa mkono na wadau mbalimbali wa soka visiwani hapa, ambao walisema
udhamini wa Grand Malt umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua soka la
Zanzibar.
Naye kocha
wa KMKM, Ally Bushiri alisema kwa sasa anahakikisha anaiandaa timu kwa ajili ya
mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Tunashukuru
kwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Grand Malt na sasa tunachofanya ni kutazama
mbele zaidi,” alisema.
Ligi Kuu ya
Zabnzibar kwa sasa inadhaminiwa na kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt,
ambao wameidhamini kwa misimu mitatu.
Post a Comment