Dar na mikoani.
Wakati
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisema CCM itazoa ushindi
katika kata zote 25 katika uchaguzi mdogo wa madiwani ambao kampeni zake
zinaendelea nchini kote, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema
watashambulia ardhini.
Hatua
ya Lowassa inakuja baada ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless
Lema kuzindua kwa mbwembwe juzi kampeni za udiwani Kata ya Makuyuni,
Monduli kwa kutumia helikopta.
“CCM ni jeshi la miguu. Tuko pamoja na wananchi na ndiyo maana tunafungua matawi kwa kishindo,” alisema Lowassa jana.
Lowassa
aliyekuwa pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Namelok
Sokoine walimrudisha CCM, Mkuu wa Wazee wa Kimasai, Samuel Soinge
aliyekuwa Chadema,walipokuwa wakimnadi Goodluck Lerunya anayewania
udiwani katika kata hiyo.
Akizindua
kampeni katika Kata ya Mbalamaziwa, wilayani Mufindi mkoani Iringa,
Kinana alisema: “Kutokana na jeshi kubwa na wafuasi tulionao na imani
inayoendelea kuonyeshwa na wananchi kuiunga mkono CCM, tuna imani
dhamira hii itafanikiwa bila shaka yoyote.
Chadema
Akihutubia
mkutano wa kampeni katika Viwanja vya Soweto Arusha juzi, Lema alisema
chama chake kimepata taarifa kuwa baadhi ya vyama vimejiandaa kufanya
fujo ili kuvuruga kampeni za Chadema inayopigana kurejesha viti vinne
vya udiwani katika Kata za Elerai, Kimandolu, Kaloleni na Themi.
“Kama
jeshi la polisi hawatatulinda, tutajilinda wenyewe kupitia Red Briged.
Tunao uwezo wa kujilinda na kuwadhibiti wenye nia ya kutuhujumu,”
alisema Lema.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas alisema jeshi hilo
limejipanga kikamilifu kudhibiti vurugu na uvunjaji wa sheria kipindi
chote cha kampeni na kuvitaka vyama vyote kuzingatia sheria, kanuni na
taratibu.
Akimnadi
mgombea wa Chadema Kata ya Kaloleni, Emmanuel Kessy, Lema aliwaomba
wapiga kura kuwachagua wagombea wa Chadema ili kukipa chama hicho uwezo
wa kuongoza Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Singida na Arusha
Akimnadi
mgombea udiwani wa CUF katika Kata ya Iseke, Tarafa ya Ihanja, Wilaya
ya Ikungi, Singida, Abdallah Kinyeje, Mwenyekiti wa chama hicho Mtaa wa
Mkunduge Kinondoni, Dar es Salaam, Tamim Omari Tamim alisema chama chake
hakina udini, ukabila, ukanda, ubaguzi, kupandikiza chuki wala harufu
ya vurugu zinazosababisha madhara na Watanzania kupoteza maisha.
CUF
pia kimetamba kuibuka na ushindi katika uchaguzi mdogo katika kata tatu
za Arusha Mjini, kati ya nne kutokana na kuwa na wagombea
wanaokubalika. Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema:
“Hapa Kaloleni hakuna ambaye hamfahamu, Abbas Mkindi... Elerai kuna John
Bayo na Themi yupo Petro Ndalivoi.”
|
Post a Comment